Kama
umewahi kukutana na taarifa mitandaoni, kwenye vyombo vya habari au kwingineko
basi ninayo majibu yote kutoka Wizara ya Fedha kuhusu ishu ya ukata wa Fedha
Serikalini Tanzania.
Hii ni
nukuu ya Kamishna Bajeti wa Wizara ya Fedha akitoa majibu ya
pesa zilikotumika >>> “Watu waliokuwa
wanaandikisha kupiga Kura, gharama zake ndizo tulizopeleka Tume ya Uchaguzi…
Kwa mara ya kwanza katika chaguzi zote zilizowahi kufanyika mwaka huu Uchaguzi
umefanywa na fedha za Watanzania.”
Kuna ukweli
kuhusu Serikali iliyotoka madarakani kumaliza pesa zote? Majibu haya hapa
>>> “Upatikanaji wa fedha uko hivi; hela zinazokusanywa leo
zinaingizwa kwenye mfuko mkuu wa Serikali Benki Kuu. Haiwezekani mtu akakomba
hela kwa sababu zile hela zinaingia kila siku na kutoka, haiwezekani mtu akombe
hela mfuko Mkuu wa Serikali… Kama kuna mtu amekomba hela msingesikia kwamba
watumishi wa Serikali wameshindwa kulipwa mshahara? Mngesikia maandamano…
tungeweza kufanya uchaguzi wetu wenyewe? vyuo vikuu wangepata hela za mikopo?…
JK hakukomba hela hazina.” >>> Kamishna John Cheyo.
Habari kwa hisani
ya Millardayo
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .
No comments:
Post a Comment