Mwenyekiti
wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe na
aliyekuwa mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia
Ukawa, Edward Lowassa, pamoja na viongozi mbalimbali wakitazama eneo ambalo
Alphonce Mawazo, huku wakiamini kifo hicho kilipangwa kutokana na kushambuliwa
eneo la wazi katika barabara kuu ya Geita - Katoro.
Msafara wa
Lowassa ukiongozwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Waziri Mkuu
Mstaafu, Frederick Sumaye, wakiwa na wabunge zaidi ya 50 na wanachama na
wafuasi wa chama hicho, walienda eneo hilo lililopo jirani na makazi ya watu na kujioneo hali
halisi.
Mwili wa
marehemu Alphonce Mawazo, unatarajiwa kuzikwa leo,Jumatatu November
30,2015,kijijini kwao Chikobe, wilayani Geita,mkoani Geita.
Marehemu Mawazo
aligombea Jimbo la Busanda alilowania
ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu,2015 na kushindwa.
Aliuawa
Novemba 14, mwaka huu ,2015 na watu wasiojulikana katika mji wa Katoro.
|
No comments:
Post a Comment