Joto la
utawala wa Rais John Magufuli limebadili utendaji kazi wa makatibu wakuu wa
wizara mbalimbali waliozoea kukaa ofisini na sasa wanafanya kazi nje ya ofisi
na kusikiliza kero za wananchi kwenye maeneo yao.
Wakati hilo
likifanyika, Ikulu jijini Dar es Salaam imesema katibu mkuu au mtumishi yeyote
wa umma atakayeshindwa kwenda na kasi na mabadiliko ya utendaji kazi katika
serikali ya awamu ya tano ajiondoe.
Tamko hilo
linalotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, alipohojiwa
jana,November 28,2015, kuhusu kutokuwapo kwa makatibu
wakuu wa wizara kadhaa kwenye ofisini zao wiki iliyopita.
Makatibu
wakuu wa Wizara kadhaa wamelazimika kuzifunga ofisi zao na kuelekea mikoani
kusikiliza kero za wananchi.
Hali ya
viongozi hao kuhama jiji na kwenda mikoani imeleta mabadiliko ya utendaji kazi
wao baada ya miaka ya nyuma kuzoeleka kutumia muda mwingi ofisini na kuacha
kazi za nje kufanywa na waziri, naibu au watendaji wengine.
Baadhi ya
wizara ambazo zilitembelewa na kukuta ofisi za katibu mkuu zikiwa zimefungwa ni
Uchukuzi, Tamisemi, Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano na Ujenzi.
Baadhi ya
wafanyakazi wa wizara hizo ambao hawakutaka majina yao yatajwe, walisema mabosi
wao kwa sasa inakuwa nadra kuonekana ofisini wakifanya kazi kwa kuogopa
kuonekana wazembe.
"Hatujawahi
kuona katibu anakwenda mikoani kama ilivyo sasa, kila siku anakwenda huku na
kule kuangalia miradi na kero za wananchi," alisema mmoja wa wafanyakazi
wa moja ya wizara hizo.
Hatuna Muda
na Katibu Mkuu Goigoi-Sefue.
Akitoa kauli
ya serikali, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, alisema kuanzia sasa
katibu Mkuu na mtendaji wa serikali ambaye anafanya kazi kwa kusuasua ajiondoe
mwenyewe.
Alisema
tayari amefanya kikao na makatibu wote kuwaeleza suala hilo na atakayerudi
nyuma hatakuwa na nafasi katika serikali ya awamu ya tano.
"Jambo
hilo tumekubaliana kwenye kikao, serikali ya awamu ya tano haitakuwa na utani
kwa wale watakaoonekana hawaendi na kasi ya Rais, sasa wanatakiwa kuchagua kama
wanataka kuendelea na nafasi zao au
la," alisema Sefue.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .
|
No comments:
Post a Comment