ASANTENI WATANZANIA:- ACT Wazalendo chawashukuru huku kikimuomba Rais Magufuli kuamuru ZEC kutangaza matokeo ya Zanzibar. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, November 11, 2015

ASANTENI WATANZANIA:- ACT Wazalendo chawashukuru huku kikimuomba Rais Magufuli kuamuru ZEC kutangaza matokeo ya Zanzibar.

Aliyekuwa mgombea wa Urais, Mama Anna Mgwira   akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mwenendo wa siasa ulivyofanyika hapa nchini pamoja na kuwashukuru baadhi ya waandishi wa habari kwa kuripoti habari waliojitokeza katika kampeni bila kujari itikadi zao katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika ofisini kwao jijini Dar es Salaam.

Katika mkutano huo wa leo November 11,2015, Mwenyekiti wa chama hicho Anna Mgwhira alitumia nafasi hiyo kuweza kuwashukuru Watanzania kwa kujitokeza kuwasuport katika kipindi chote cha kampeni na kukifanya chama kuzidi kuwa imara zaidi.

Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini  kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe,(kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,November 11,2015, kuhusiana na kushinda kwa chama chake katika jimbo la Kigoma Mjini pamoja na Kuongoza kupata madiwani katika kata 50 hapa nchini na katika  Manispaa ya Kigoma Ujiji kufanikiwa kuunda baraza la madiwani  ikiwa  Manispaa hiyo ina kata 18  chama cha ACT-Wazalendo  kushinda na kupata madiwani 12 na CCM ikipata kata 5 na  Chadema kata 1 ikiwa kata moja haikufanya uchaguzi na itafanya Jumapili Ijayo.

Zitto Kabwe naye alizungumzia mambo mbalimbali ikiwemo kumpongeza Mwenyekiri wake Mama Anna Mgwhira kwa kumsaidia kukitangaza chama hicho na kupandisha taswira ya chama chao mbele ya umma.

Kazi iliyopo mbele yetu ni kukijenga chama na kukifanya kifike mbali zaidi, tumefanikiwa kupata kiti kimoja cha ubunge lakini tutatumia kiti hicho kupaza sauti ndani ya bunge..ikumbukwe sisi tulisema waziwazi kuhusu rushwa tofauti na vyama vingine vya upinzani ambavyo havikuwa wazi”..Zitto.

Pia alizungumzia suala ya dawa za kulevya“Nchi nyingi zimeanza kufanya mabadiliko kuhusu dawa za kulevya, dunia nzima imeanza mkakati wa kupambana na dawa za kulevya, ujangili pamoja na rushwa ambayo ndio mambo tutakayokwenda nayo ndani ya bunge ili kuweza kupaza  sauti zetu ndani ya jamii inayotuzunguka”...
Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama cha ACT -Wazalendo, Samson Mwigamba katikati ni aliyekuwa mgombea wa Urais wa chama cha ACT-Wazalendo,Mama Anna Mgwira na kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini  kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,November 11,2015.

 Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe ,pia alimpongeza Rais Dk.Magufuli kwa kuweza kudhibiti safari za njeWakati nikiwa Mwenyekiti wa PAC niliagiza kufanywa ukaguzi wa fedha za umma kuhusu safari za nje za viongozi wetu, nataka tu niwahahakikishie Watanzania wenzangu mimi na marehemu Deo FILIKUNJOMBE tuliagiza ukaguzi na upo tayari, wakati wowote tutawaita na kulitolea maelezo ya kina”.

Kwenda tu katika sehemu na kushtukiza hakutatatua wizi wa mali za umma, tunataka Rais aweke mifumo endelevu ili leo na kesho akiwa hayupo iweze kufanya kazi kwa manufaa ya umma”.

Kuhusu mgogoro wa Zanzibar Zitto amesema “ZEC imefuta uchaguzi lakini ukisoma katiba ya Zanzibar hakuna mahali panaonyesha Mwenyekiti wa Zanzibar ana mamlaka ya kufuta uchaguzi, kama tatizo lilikuwa ni majimbo ya Pemba tume ilipaswa kurudia kuhesabu kura kwenye yale majimbo husika”.

Mpaka leo tunapozungumza kikatiba Zanzibar haina Serikali, mtu yeyote anayejiita rais wa Zanzibar kikatiba amepindua, anapaswa kushtakiwa kwa kosa la kiuhaini na kosa lake adhabu yake ni kifo, tunamtaka Rais Magufuli ahakikishe tume ya ZEC inatangaza matokeo”.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhulia katika mkutano na viongozi wa chama cha ACT-Wazalendo jijini Dar es Salaam leo.

Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad