Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete usiku wa Ijumaa, Oktoba
23, 2015, amewateua Makatibu Wakuu wanne wapya wa wizara mbali mbali.
Aidha, Rais Kikwete amewateua Naibu Makatibu Wakuu wapya watano, amewateua
Makatibu Tawala wa Mikoa wawili na pia amewahamisha Naibu Makatibu Wakuu
wawili.
Kwa mujibu wa uteuzi huo,Rais Kikwete amemteua Ndugu Hab Mkwizu kuwa
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma; Profesa Elisante
Ole Gabriel kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo;
Dkt. Yamungu Kayandabila kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia na Mhandisi Omari Chambo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na
Madini.
Aidha, kwa mujibu uteuzi huo, Rais Kikwete
amemteua Mhandisi Paul M. Masanja kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na
Madini; Dkt. Maria Mashingo kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi
na Ndugu Zidikheri M. Mundeme kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Chakula
na Ushirika.
Wengine walioteuliwa kuwa Naibu Makatibu
Wakuu ni Ndugu Tixon T. Nzunda ambaye anakuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Ndugu Emmanuel Kalobelo ambaye anakuwa Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.
Walioteuliwa kuwa Makatibu Tawala wa Mikoa ni
Ndugu Eliakim Maswi ambaye anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara na Mhandisi
Madeni Kipande ambaye anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi.
Katibu Mkuu ambaye anahamishwa ni Bibi Sihaba Nkinga ambaye anakwenda kuwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Wanawake, Jinsia na Watoto kutoka Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo.
Naibu Makatibu Wakuu wanaohamishwa ni Ndugu
John T. Mngodo ambaye anahamishiwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya kutoka Wizara ya
Uchukuzi na Ndugu Mwamini Juma Malemi ambaye anakwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu,
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Wateuliwa hao wote wataapishwa asubuhi ya
leo, Jumamosi, Oktoba 24, 2015, Ikulu mjini Dar es Salaam.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment