Nape Nnauye.
Jimbo la Mtama: Mgombea ubunge wa Jimbo la Mtama kupitia CCM, Nape Nnauye ameibuka mshindi katika jimbo hilo. Nape ameshinda kwa jumla ya kura 28110, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Suleiman Luwongo wa CHADEMA, aliyepata kura 13918. Jimbo la Ubungo: Mgombea Ubunge Jimbo la Ubungo kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Saed Kubenea ameshinda ubunge wa jimbo hilo akimwangusha mpinzani wake Dk. Didas Masaburi wa CCM. Jimbo la Kigamboni: Mgombea ubunge Jimbo la Kigamboni, Dk. Faustine Ndugulile (CCM) ameshinda ubunge wa jimbo hilo na kufanikiwa kutetea kiti chake. Jimbo la Singida Magharibi: Kingwi Immanuel wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 25102, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Allute Mdinka wa Chadema, aliyepata kura 13480 Jimbo la Singida Mashariki: Tundu Lissu wa Chadema, ameshinda kwa jumla ya kura 25010, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Jonathan Njau wa CCM, aliyepata kura 18614. Jimbo la Singida Mjini: Mussa Sima wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 36690, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Mgana Msindai wa Chadema, aliyepata kura 16702 Jimbo la Ismani: Wiliiam Lukuvi ametangazwa kuwa mshindi kwa kiti cha Ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Ismani, mkoani Iringa kwa kuwa na jumla ya kura 26,119 na mpinzani wake Patrick Sosopi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kushindwa kwa kupata jumla ya kura 15,534 Jimbo la Ndanda: Cecil Mwambe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) apata kiti cha Ubunge katika Jimbo la Ndanda mkoani Mtwara kwa kuwa na kura 26,247, huku Mariam Kasembe wa Chama cha Mapinduzi kukikosa kiti hiko kwa kupata kura 26,215 Jimbo la Same Magharibi: Dkt. David Mathayo wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 21418, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Christopher Sangweli wa Chadema, aliyepata kura 15347 Jimbo la Same Mashariki: Naghenjwa Livingstone Kaboyoka wa Chadema, amembwaga Anne Kilango Malecela kwa kupata kura 18836, dhidi ya kura 15539 za Anne. Jimbo la Mbogwe: Augustino Manyanda wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 32921, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Maganga Nicodemas Henry wa Chadema, aliyepata kura 13975 Jimbo la Mtwara Mjini: Maftah Nachuma wa Chama cha CUF ameshinda kwa kura za Ubunge, huku Asnain Murji kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) ameshindwa kukitetea kiti chake Jimbo la Hai: Freeman Mbowe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) atangazwa kuwa Mbunge kwa kupata jumla ya kura 51,124, huku mgombea kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Danstan Mallya apata jumla ya kura 26,966.
Jimbo la Ngara: Alex Gashaza wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura
53387, dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Dkt.Peter Bujari wa Chadema aliyepata
kura 35254
|
Zitto
Kabwe.
Jimbo la Iramba Magharibi: Mwigulu Nchemba wa CCM, aibuka mshindi kwa jumla ya kura 54660, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Jesca Kishoa wa Chadema aliyepata kura 12580 Jimbo la Ileje: Janet Mbene wa CCM, aibuka mshindi kwa jumla ya kura 27582, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Emmanuel Mbuba wa NCCR-Mageuzi, aliyepata kura 14578 Jimbo la Mpanda Mjini: Sebastian Kapufi wa CCM, aibuka mshindi kwa jumla ya kura 29193, dhidi ya mpinzani wake wa karibu wa Chadema Jonas Kalinde, aliyepata kura 18649 Jimbo la Njombe Kaskazini: Joram Hongoli (CCM) akishinda Jimbo la Njombe Kaskazini. Jimbo la Dodoma Mjini: Anthony Mavunde (CCM) ametangazwa kuwa mshindi wa ubunge Jimbo la Dodoma Mjini. Jimbo la Bukombe: Dotto Biteko (CCM) ameshinda ubunge Jimbo la Bukombe. Jimbo la Kondoa Mjini: Edwin Sanda (CCM) ametangazwa mshindi Jimbo la Kondoa Mjini. Jimbo la Chato: Dk Medad Kalemani Jimbo la Chato (CCM) ametangazwa mshindi baada ya kupata kura 78817 dhidi ya mpinzani wake Benedicto Lukanima (Chadema) akipata kura 32513.
Jimbo la Bukoba Mjini: Mgombea ubunge wa Jimbo la Bukoba Mjini kupitia
Chadema, Wilfred Lwakatale ameibuka mshindi katika jimbo hilo
kwa kumshinda mpinzani wake Khamis Kagasheki.
|
Joseph
Mbilinyi (Sugu).
Jimbo la Mchinga: Hassan Bobali wa CUF, ameshinda kwa jumla ya kura 14776, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Saidi Mtanda wa CCM, aliyepata kura 13665 Jimbo la Sumbawanga Mjini: Aeshi Hilaly wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 41763, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Ikuwo Malila wa Chadema, aliyepata kura 36183. Jimbo la Lupembe: Joram Hongoli wa Chama cha Mapinduzi (CCM) atangazwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Lupembe kwa kupata jumla ya kura 20,430 na kumwangusha mpinzani wake toka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Edwin Swalle aliyepata jumla ya kura 10407 Jimbo la Kasulu Mjini: Mgombea ubunge jimbo la Kasulu Mjini kupitia chama cha CCM, Daniel Sanze ametangazwa kuwa mshindi wa jimbo hilo katika uchaguzi mkuu uliofanyika jana huku akimbwaga mpinzani wake Moses Machali wa ACT Wazalendo aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo. Moses Machali amepata kura 22,512 wakati Daniel wa CCM amepata kura 25,336. Jimbo la Kahama Mjini: Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kahama Mjini (CCM), Jumanne Kishimba (CCM), ametangazwa kuwa mshindi wa jimbo hilo katika uchaguzi mkuu uliofanyika October 25,2015.
Jimbo la Monduli: Mgombea Ubunge wa Jimbo la Monduli (CHADEMA), Julius
Kalenga ametangazwa kuwa mbunge wa jimbo hilo.
|
Hussein
Bashe.
Jimbo la Ilemela: Mgombea Ubunge Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza, Angelina Mabula (CCM) ametangazwa rasmi mshindi wa jimbo hilo kwa kumbwaga mpinzani wake aliyekuwa mbunge ya jimbo hilo, Highness Kiwia (Chadema). Tarifa zaidi zinasema Kiwia hakuwepo wakati wa kutangazwa matokeo hayo. Jimbo la Moshi Mjini: Mgombea Ubunge Jimbo la Moshi Mjini, Japhary Raphael Michael (CHADEMA) ametangazwa rasmi mshindi wa jimbo hilo kwa kupata jumla ya kura 51656 na kumuangusha Davis Mosha wa CCM. Jimbo la Bunda Mjini: Mgombea Ubunge Jimbo la Bunda Mjini, Ester Bulaya (CHADEMA) ametangazwa rasmi mshindi wa jimbo hilo na kumuangusha Steven Wasira. Jimbo la Siha: Mgombea Ubunge wa Jimbo la Siha kwa tiketi ya CHADEMA/UKAWA, Dk. Godwin Mollel,ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa jimbo hilo.
Arumeru Mashariki: Joshua Nassari wa Chadema ameshinda ubunge
Jimbo la Arumeru Mashariki akipata kura 86694.
|
Ester
Matiku.
Lindi Mjini: Hassan Suleiman Kaunje (CCM) ametangazwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi Manispaa ya Lindi, kuwa Mbunge Mteule wa Jimbo la Lindi Mjini.
Mbinga Vijijini: Mgombea Martin Msuha (CCM) ametangazwa rasmi na
Msimamizi wa Uchaguzi, Venance Mwamengo kuwa mshindi wa ubunge katika Jimbo la Mbinga Vijijini baada ya kupata
kura 59,269.
|
Sixtus
Mapunda.
Tunduma: Mgombea Mwakajoka Frank (Chadema) ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa ubunge katika Jimbo la Tunduma (Mbeya) akipata kura 32,442. Matokeo hayo yametangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi Halima Mpita. Tandahimba: Mgombea Ubunge wa CUF katika Jimbo la Tandahimba mkoani Mtwara, Ahmed Katani ametangazwa kuwa mshindi wa jimbo hilo. Musoma Mjini: Mgombea Vedatus Mathayo (CCM) ametangazwa rasmi na Msimamizi wa Uchaguzi kuwa mshindi wa ubunge katika Jimbo la Musoma Mjini baada ya kupata kura 32,836. Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630. |
No comments:
Post a Comment