Ofisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la
Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph, akizungumza
katika kongamano lililowakutanisha watendaji kutoka Redio za jamii
nchini katika mji wa Terat, wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara jana.
Mwenyekiti
wa Muungano wa Redio za Kijamii nchini (COMNETA), Sekiku Joseph
akizungumza katika Kongamano hilo ambalo amesisitiza umuhimu wa viongozi
wa Radio za kijamii kuthamini michango inayotolewa na wafadhili ili
iweze kuwa endelevu.
Mshauri
na Mkufunzi wa masuala ya vyombo vya habari jamii kutoka Shirika la
Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji
Mwalimu akisistiza jambo katika mafunzo hayo.
Afisa Miradi mpya wa Unesco, Nancy Kaizirege akisisitiza jambo.
Mkurugenzi
wa Redio ya Jamii Uvinza FM, Ayub Kalufya akichangia mada na kuomba
Unesco kuendelea kutoa usaidizi kwao kutokana na mchango wanaoutoa kwa
jamii.
Afisa
Miradi mpya wa Unesco, Nancy Kaizirege akisisitiza jambo wakati mafunzo
hayo yakiendelea. kulia ni Meneja wa Orkonerei Radio Service Simanjiro
Manyara (ORS FM), Bw.Baraka Ole Maika.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Redio ya Jamii 94.9 FM , Mkoani Pemba, Hamidu Hassan Bakari
akizungumza namna Redio yake itakavyonufaika kupitia mafunzo ya
kuwajengea uwezo na vifaa ya matangazo.
Meneja wa Redio Kahama FM, Marco Mipawa, akizungumza jambo.
Mwandishi Wetu,Simanjiro
Shirika
la Umoja wa Mataifa la Elimu,Sayansi na Utamaduni(UNESCO) limeendelea
kuimarisha Redio za Jamii nchini kwa kuwapa mafunzo ya mara kwa mara
watendaji wa ngazi mbalimbali kwa lengo la kuzifanya Redio hizo
kuwahudumia vema wananchi wanaoishi maeneo ya vijijini.
Ofisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la
Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph amesema
kumekuwa na mafanikio tangu mradi huo kuanza miaka mitatu iliyopita
chini ya ufadhili wa UNESCO, Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) na
Serikali ya Uswizi ambapo licha ya kuwajengea uwezo vifaa vya
kieletroniki vilitolewa kwa Redio hizo.
Kongamano
hilo la mwaka la siku tatu(3) linafanyika katika Kituo cha Orkonerei
Radio Service Simanjiro Manyara (ORS), Terat wilayani Simanjiro mkoa wa
Manyara na limewaleta pamoja watendaji wa Redio za Jamii 20 kutoka mikoa
mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar .
“Tunalenga
kuwajengea uwezo ili hizi Redio za Jamii zifanye kazi kwa weredi ya
kuleta maendeleo endelevu kwa wananchi waweze kushiriki mijadala
inayohusu sekta za afya, elimu na kilimo,”amesema Yusuph
UNESCO inafanya kazi kwa karibu na Muungano wa Radio za Kijamii Tanzania(COMNETA)unaongozwa na Mwenyekiti wake Sekiku Joseph.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
No comments:
Post a Comment