Baadhi ya
wanafunzi wa shule ya msingi Uhuru mchangayiko na wadau mbalimbali wa
maendeleo, waandishi wa habari wakiwa kwenye picha ya pamoja na vibao vya
malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
|
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez (kulia) na Mwakilishi Mkazi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UN Women nchini Tanzania, Anna Collins-Falk
(katikati) wakipata picha ya kumbukumbu sambamba na mmoja wa wadau wa
maendeleo. (Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Na Mwandishi wetu
UMOJA wa Mataifa kwa kushirikiana na Serikali
ya Tanzania wamezindua rasmi malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
Malengo hayo ambayo pia yanajulikana kama
malengo ya dunia yamezinduliwa Septemba 29 katika hoteli ya Serena jijini Dar
es salaam.
Uzinduzi huo ulifanywa na Mratibu wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez,
Kamishina wa mipango (POPC) Bw. Paul Kessy, na Kamishina wa Mipango wa
Zanzibar, Bw. Ahmed Makame kwa niaba ya serikali, Bi. Fionnuala Gilsenan,
Balozi wa Ireland na Bi. Liz Lloyd, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya
Standard Chartered Tanzania kwa niaba ya wadau wa mradi wa Project Everyone
Partners.
SDGs ni wito wa dunia wa kuchukuliwa kwa
hatua za kuufuta umaskini, kuihami dunia dhidi ya uharibifu wa mazingira na
kuhakikisha kwamba kila mwanadamu anaishi maisha stahiki katika amani na
ustawi.
Katika malengo hayo 17 yapo makusudio 169
yanayotoa ramani ya utengenezaji wa sera za maendeleo na namna ya kutekeleza
kwa miaka 15 ijayo.
Malengo hayo yakijengwa juu ya mafanikio ya
malengo ya milenia (MDGs), yameingiza vitu vipya kama mapambano dhidi ya
tofauti za kiuchumi, ubunifu, mabadiliko ya tabia nchi, lishe, amani na haki.
SDGs ni mpango wa dunia unaojikita kwa ustawi wa wanancni na dunia.
|
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP), Awa Dabo (kushoto) na Kiongozi wa mabalozi wa nchi za nje hapa nchini
Mheshimiwa Juma Mpango, ambaye ni balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
(DRC) wakiwa wameshikilia lengo namba 16 na 17 kati ya malengo 17
ya Maendeleo Endelevu ya Dunia ambayo yamezinduliwa rasmi nchini
Tanzania 29, Septemba 2015.
Akizungumza umuhimu wa malengo hayo,
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa UNDP Bw.
Alvaro Rodriguez amesema: “Kwa mara ya kwanza katika historia ya dunia ,
serikali zimekutana na kukubaliana kupeana malengo kwa ajili ya kila mtu.
Malengo haya yatasaidia mataifa yote kushirikiana katika kuwezesha ustawi,
kupunguza matumizi na kuilinda dunia dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.
Katika
hilo watashughulikia elementi zinazohusu maendeleo endelevu: ukuaji wa uchumi,
ustawi wa jamii na kulinda mazingira.”
Akizungumzia malengo hayo Bw. Paul Kessy
amesema kwamba serikali ya Tanzania ipo tayari kwa malengo hayo.
Alisema kwamba Rais Jakaya Kikwete
alikuwa New York, Marekani kwa ajili ya kutia saini malengo hayo na hilo
linaonesha ni kiasi gani serikali ya Tanzania iko tayari kushirikiana na wadau
wengine kuufuta umaskini.
Pia alisema:“Wakati huu, masuala ya
uimarishaji wa muundo wa utekelezaji na kuamsha upya ushirikiano wa kidunia
katika maendeleo ni msingi mzuri”
Naye Kamishina wa mipango wa Zanzibar,
Bw Ahmed Makame : “Nikiangalia malengo haya 17 ya SDGs, ninafuraha kuona kwamba
Zanzibar imekuwa sehemu ya mchakato huu...”.
|
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard
Chartered Tanzania, Bi. Liz Lloyd akipozi kwa picha na lengo na tisa kabla
ya uzinduzi rasmi wa Malengo ya Dunia kwa Maendeleo Endelevu.
Aidha alisema kwamba Tanzania imeanza vyema
katika utekelezaji wa malengo hayo.
Alisema kwa kuangalia uzoefu uliopatikana
katika malengo ya milenia, inaonekana namna bora ya kuuoanisha malengo ya
kitaifa na ya dunia.
Ninafurahi kusema kwamba Zanzibar tuko katika
mchakato wa kutengeneza mkakati wa maendeleo wa kitaifa na tumepanga kufikia
malengo ya SDGs.
Akisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika
kufanikisha maendeleo, Bi.Fionnuala Gilsenan, amesema taifa lake Ireland
lipo tayari kusaidia kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu.
“Malengo ya dunia yaliyojengwa katika
Malengo ya Milenia yamelenga kukabiliana na matatizo ya zamani kwa mbinu mpya.
Zimelenga kukabiliana na tatizo la umaskini na ukosefu wa usawa katika masuala
ya uchumi. SDGs haiwezi kufanikiwa bila kuyaangalia masuala ya mabadiliko ya
tabia nchi, usawa wa jinsia, haki za biandamu na kukabiliana na mfumo
inayobagua.”
Akizungumza kwa niaba ya wadau wa Project
Everyone, Bi. Liz Lloyd alielezea umuhimu wa sekta binafsi kushirikiana na
Umoja wa Mataifa na serikali ya Tanzania katika kusambaza ujumbe wa malengo ya
dunia.
|
Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO),
nchini Tanzania, Dk.Rufaro Chatora akipozi la lengo namba 3.
“Kama benki huwa tunazungumza na
umuhimu wa kuendelea kuwapo.
Huu si tu msemo bali ahadi tunayoishi nayo kila
siku. Malengo ya Dunia yanatoa nafasi adhimu ya ushirikiano na taasisi kubwa
duniani, kutekeleza malengo 17 kwa nia ya kufufua ushirikiano wa dunia kwa
maendeleo endelevu.
Standard Chartered inajisikia furaha ya
kuwa nchini Tanzania kwa miaka mingi na inatumaini kwamba kwa ushirikiano huu
kila mtu anayeishi nchini hapa atafaidika na maendeleo endelevu ya
kiuchumi na kijamii.”
Malengo ya Maendeleo Endelevu yalizinduliwa
Septemba 25 wakati viongozi wa dunia walipokutana pamoja mjini New York.
Malengo haya yataanza kutumika Januari 1,2016.
|
Mkuu wa
ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Peter
Malika akipozi na lengo na 17.
|
Mratibu wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez
katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa kabla ya uzinduzi rasmi wa
malengo hayo nchini Tanzania.
|
Mtaalam wa
mawasiliano kutoka UNFPA, Sawiche Wamunza (kushoto) sambamba na Afisa Habari wa
kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama katika picha
ya ukumbusho.
|
Meza kuu
katika halfa ya uzinduzi wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs) nchini
Tanzania, kutoka kushoto ni Mtaalamu wa masuala ya uchumi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Dar es salaam, Rogers Dhliwayo, Balozi
wa Ireland nchini Tanzania, Mh.
Fionnuala Gilsenan, Kamishina wa mipango (POPC) Bw. Paul Kessy, Mratibu wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez,
Kamishina wa Mipango wa Zanzibar, Bw. Ahmed Makame pamoja na Ofisa Mtendaji
Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Bi. Liz Lloyd.
|
Mratibu wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez,
akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 (
SDGs).
|
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Bi. Liz Lloyd akielezea
ushiriki wa benki yake katika utekelezaji wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 (
SDGs).
|
Kamishina wa
mipango (POPC) Bw. Paul Kessy akizungumza kwa niaba ya serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwenye hafla ya uzinduzi wa malengo ya Maendeleo Endelevu
17 ( SDGs).
|
Kamishina wa
Mipango wa Zanzibar, Bw. Ahmed Makame akiwakilisha serikali ya Mapinduzi
Zanzibar.
|
Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mh. Fionnuala
Gilsenan akizungumza kwenye hafla hiyo ambapo alisisitiza umuhimu wa
ushirikiano katika kufanikisha maendeleo.
|
Baadhi ya
wadau wa maendeleo kutoka mashirika na balozi mbalimbali waliohudhuria uzinduzi
wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs) iliyofanyika jana jijini Dar es
Salaam.
|
Baadhi ya
wageni waalikwa na wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania
wakifuatilia maoni na maswali yaliyokuwa yakiwasilishwa kwenye hafla hiyo.
|
Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR),
Joyce Mends-Cole akijibu moja ya swali lililoulizwa na kijana (hayupo pichani).
|
Sehemu ya
wadau wa Maendeleo, taasisi mbalimbali, asasi za kiraia, waandishi wa habari
waliohudhuria uzinduzi huo.
|
Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA),
Dkt. Natalia Kanem akifafanua jambo katika kipindi cha maswali na majibu.
|
Mratibu wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez
(kulia), Kamishina wa Mipango wa Zanzibar, Bw. Ahmed Makame ( wa pili kulia),
Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mh.
Fionnuala Gilsenan (kushoto) Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya
Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahaya (wa pili kushoto) kwa pamoja
wakifunua pazia maaluma kuashiria uzinduzi rasmi wa malengo ya Maendeleo
Endelevu 17 ( SDGs).
|
Meza kuu
katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Uhuru mchangayiko
walioshiriki kutengeneza tangazo maalum la kuelimisha jamii kuhusiana na
malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
|
Meza kuu
katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
|
Meza kuu
katika picha ya pamoja na baadhi ya waandishi wa habari akiwemo Mwanahabari
mkongwe Mama Eda Sanga walioshiriki kwenye uzinduzi huo.
|
Bendera ya
Umoja wa Mataifa, SDG's na bendera za
nchi mbalimbali zikipepea kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
|
No comments:
Post a Comment