UCHAGUZI MKUU TANZANIA 2015 - 2020:-Dk. John Pombe Magufuli ndiye Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, October 29, 2015

UCHAGUZI MKUU TANZANIA 2015 - 2020:-Dk. John Pombe Magufuli ndiye Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha CCM John Pombe Magufuli  ndiye rais mteule wa taifa la Tanzania baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Jumapili,October 25, 2015.



Akitoa matokeo hayo mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa Magufuli alijipatia kura 8,882,935 ikiwa ni aslimia 58.46 huku mpinzani wake wa karibu Edward Lowassa wa chama cha Chadema akijipatia kura 6,072,848 ikiwa ni asilimia 39.97 ya kura zote.

Kwa  Mujibu  wa  jaji  Lubuva, Dr  magufuli  amepata  ushindi  wa  kura Milioni 8 ( 8,882,935  ) sawa  na  asilimia  58.46%  huku  akimwacha  kwa  mbali  mpinzani  wake  wa  karibu , Edward  Lowassa (Chadema )  ambaye  amepata  jumla  ya  kura  Milioni 6 (  6,077,848  )  sawa  na  asilimia  39.97%

Dr  Magufuli  na  mgombea  mwenza, Bi Samia Suluhu  watakabidhiwa  rasmi  vyetu  vya  ushindi  kesho ,October 30,2015 saa  nne  asubuhi  katika  ukumbi  wa  hoteli  ya  Diamond  Jubilee  .
Matokeo ya uchaguzi wa urais Tanzania
JinaChamaKuraAsilimia
Anna MghwiraACT98,7630.65
Chifu YembaADC66,0490.43
John MagufuliCCM8,882,93558.46
Edward LowassaCHADEMA6,072,84839.97
Hashim SpundaCHAUMA49,2560.32
Janken KasambalaNRA8,0280.05
Macmillan LyimoTLP8,1980.05
Fahmi DovutwaUPDP7,7850.05
Awali kabla ya kutolewa kwa matokeo hayo vyama vya siasa vilivyokubaliana na matokeo vilitia sahihi matokeo hayo.

 Lakini chama cha Chadema, chake Bw Lowassa hakikuwakilishwa. Chama hicho kimepinga matokeo hayo.

Akivihutubia vyombo vya habari mgombea wa urais kupitia chama hicho Edward Lowassa amepinga matokeo yoyote ya uchaguzi huo na kujitangaza mshindi wa uchaguzi kwa kupata asilimia 62 ya kura zilizopigwa.

Lowassa amedai kwamba tume ya uchaguzi nchini humo imeshirikiana na chama tawala CCM kufanya udanganyifu katika shughuli hiyo, madai ambayo tume hiyo imekanusha.

"Hatuna hata chembe ya wasiwasi kwamba mchakato huu ulifuata sheria na ni halali," alisema Jaji Lubuva muda mfupi kabla ya kutangaza matokeo.

Aidha, amesema tume iliendesha mchakato wote "bila shinikizo".


Akizungumzia kutoidhinishwa kwa matokeo hayo na wawakilishi wa Chadema, mkurugenzi wa uchaguzi katika tume Bw Ramadhan Kailima alisema sheria inawaruhusu kuendelea na kutangaza matokeo hata bila chama chochote kile kuwakilishwa au kuidhinisha matokeo husika.

Kwenye uchaguzi huo, kati ya wapiga kura 23,161,440 waliojiandikisha, ni 15,589,639 waliopiga kura, ambao ni asilimia 67.31 ya wapiga kura wote. Kura 402,248 ziliharibika.

Kufuatia kutangazwa kwa matokeo hayo, tume hiyo ya uchaguzi sasa inatarajiwa kumkabidhi Bw Magufuli cheti cha kuwa mshindi wa urais.

Muda mfupi baada ya kutangazwa kwa matokeo, chama hicho kimeanza kusherehekea kwenye mtandao wa Twitter huku wafuasi wake nao wakianza kusherehekea katika barabara za miji.

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad