Tuzo
hizo ambazo zilikuwa maalumu mwaka huu, kwani zimetumika kumuaga Rais Kikwete kwa kumaliza muda wake madarakani na
kuheshimu mchango wake katika kuinua michezo nchini katika kipindi cha utawala
wake. Ikumbukwe kuwa Tuzo hizo ziligawanyika katika vipengele vinne, Taasisi
iliyochangia kuinua michezo katika kipindi cha miaka kumi Tuzo 5.
|
Tuzo
zimetolewa kwa wanamichezo waliofanya vizuri katika kipindi cha miaka kumi,
viongozi waliochangia kuinua michezo katika kipindi cha miaka kumi Tuzo 5 na
Tuzo ya heshima kwa Mh Rais Jakaya Mrisho
Kikwete kwa kuheshimu mchango wake katika kuinua michezo wakati
wa utawala wake, baadhi ya waliopewa Tuzo usiku wa October 12 ni Francis Cheka, Mbwana Samatta, Iddi Kipingu, Abdallah Majura na Hashim Thabiti.
|
Mama yake
Hashim Thabiti akichukua Tuzo kwa niaba ya Hashim.
|
Charles
Mkwasa akichukua Tuzo ya Twiga Stars kwa kufanya vizuri katika kipindi cha
miaka 10.
|
Wawakilishi
wa Mbwana Samatta wakichukua Tuzo kwa niaba yake
|
Kanali Iddi
Kipingu akipokea Tuzo yake ya heshima kwa kusaidia kuinua michezo kwa muda
mrefu toka yupo shule ya Makongo
|
Rais Kikwete
akimkabidhi tuzo Dioniz Malinzi kwa kujenga Uwanja wa Gofu Misenyi mkoani
Kagera
|
Rais wa
zamani wa TFF Leodger Tenga kapata Tuzo ya kiongozi bora katika kuinua michezo
|
Abdallah
Majura akikabidhiwa Tuzo ya heshima katika kuinua michezo sasa kafungua kituo
cha Radio kinachojihusisha na michezo.
|
Mzee Said
akipokea Tuzo ya Taasisi iliyochangia kuinua michezo nchini Azam SSB
|
Mwenyekiti
wa TASWA Juma Pinto akimkabidhi Rais Kikwete Tuzo ya heshima akiwa pamoja na
mkuu wa mkoa Dar Es Salaam Meki Sadiki, waziri wa michezo Dk Fenella Mukangara
na Dioniz Malinzi.
|
Nahodha wa
Taifa Stars Nadir Haroub akikabidhi jezi ya Taifa Stars kwa Rais Kikwete ikiwa
imesainiwa na wachezaji wote.
|
Baada ya
ugawaji wa Tuzo Rais Kikwete alipata nafasi ya kuongea na waandishi wa habari
na wageni waalikwa katika Tuzo hizo.
|
Rais Kikwete
katika picha ya pamoja na watu mbalimbali.
|
Rais Kikwete
katika picha ya pamoja na washindi wa Tuzo hizo.
|
Yamoto Band
wakaitimisha kwa kuwachezesha waandishi wa habari kimadoido
|
No comments:
Post a Comment