Marehemu
Christopher Mtikila enzi za uhai wake.
Mnamo tarehe 04/10/2015 majira ya
saa 05:45hrs huko Msolwa Kata ya Bwilingu barabara kuu ya Dar es Salaam –
Morogoro, Wilaya ya Ki-Polisi Chalinze, Mkoa wa Pwani. Gari No. T.189 AGM aina
ya Toyota Corolla likiendeshwa na George Steven Ponera miaka 31, mkazi wa Mbezi
Mwisho Dar es Salaam liliacha barabara kisha kupinduka na kusababisha kifo cha
Christopher Mtikila miaka 62, mpangwa, mchungaji wa Kanisa la Assemblies, na
mwenyekiti wa Chama cha siasa DP mkazi wa Kinondoni “B” Dar Salaam.
Katika ajali hiyo, watu watatu
waliokuwamo ndani ya gari hilo na marehemu Mchungaji Mtikila walijeruhiwa ambao
ni Ally Mohamed miaka 42 mkazi wa Mbezi Dar es Salaam, yeye alipata maumivu
shingo, mabegani na kifuani, mwengine ni Patrick Mgaya miaka 37 ambaye ni
mchungaji wa Kanisa la Assemblies of God mkazi wa Mbagala Dar es Salaam ambaye
alikuwa na michubuko midogo usoni na kuumia kichwani, pamoja na George Steven
miaka 31 mkazi wa Mbezi Dar es Salaam ambaye alipata michubuko kidogo eneo la
mabegani.
Majeruhi wote walipatiwa matibabu katika Kituo cha afya Chalinze na
badae wawili kati yao katika Hospitali teule ya Tumbi na waliruhusiwa kutokana
na hali zao kuendelea vizuri.
Baada ya kutokea kwa hiyo ajali,
timu maalum ilifika katika eneo la tukio kwa ajili ya ufuatiliaji wa ajali hiyo
ikiongozwa na Mkuu wa utawala wa Traffic kuu Dar es Salaam SACP J. Kahatano,
pamoja na mimi mwenyewe, Mkuu wa Upelelezi Makosa ya Jinai Mkoa wa Pwani na
kuwashirikisha wataalamu wa Forensic Makao Makuu ya Polisi ACP Kashindye na
Dokta A. Makata.
Uchunguzi wa mwili wa marehemu
tayari umefanyika, na taarifa ya Daktari aliyefanya uchunguzi huo katika
Hospitali ya Rufaa tumbi Kibaha jana tarehe 04/10/2015 umeonyesha kuwa, kifo
cha marehemu kimesababishwa na kuvunjika kwa mbavu nane (8) upande wa kushoto
na kuingia kwa damu kwenye mfumo wa hewa na kusababisha kushindwa kupumua.
Kabla ya ajali hiyo kutokea marehemu
na wenzake tarehe 02/10/2015 jioni waliondoka Dar es Salaam kwenda Mkoa wa
Njombe na kufika tarehe 03/10/2015 alfajiri kwa ajili ya kampeni za Chama chao
cha DP. Wakiwa huko walipata ajali kwa kugonga magari mawili yaliyopata ajali
na kusababisha uharibifu wa gari lao.
Kulingana na taarifa ya Mkaguzi wa
magari ya tarehe 03/10/2015 huko Njombe walishauriwa walitengeneze kwanza kabla
ya kulitumia tena.
Tarehe 03/10/2015 saa 21:30hrs
waliondoka Njombe kwenda Dar es Salaam na ilipofika saa 05:45hrs katika eneo la
Msolwa ndipo wakapata ajali hii.
Uchunguzi uliofanywa kwa kukagua
tukio na kuwahoji majeruhi walionusurika (katika eneo hilo hakuna watu wengine
walioshuhudia tukio hilo kwa kuwa si eneo la makazi ya watu, ni mbuga).
Ajali
hii imeonyesha kuwa imesababishwa na sababu zifuatazo:-
1.
Mwendo kasi, dereva mwenyewe
anakubali kwamba alikuwa mwendo kasi licha ya kuwepo kwa alama zinazooonyesha
kwenda mwendo wa Km 50 kwa saa.
Aidha baada ya kuacha barabara kuu, gari hilo
lilikwenda umbali wa mita 125 kabla ya kupinduka hali inayoashiria kuwa
lilikuwa kwenye mwendo kasi.
2.
Uchovu wa dereva kutokana na safari
ndefu kwa kuendesha gari mchana na usiku kucha kabla ya kuanza safari walikuwa
wakishughulikia matengenezo ya gari hilo ambapo hakupata muda wa kupumzika.
3.
Kutofunga mkanda ya usalama. Katika
uchunguzi inaonyesha marehemu hakufunga mkanda kwa kuwa alirushwa nje kupitia
kioo cha mbele (wind screen).
4.
Ubovu wa gari. Gari hilo lilipata
ajali tarehe 03/10/2015 na moja ya sehemu muhimu iliyoharibika ni mfumo wa
usukana (steering system) yawezekana halikupata matengenezo kikamilifu na hivyo
kuchangia kutokea kwa ajali hiyo.
Hivyo nitumie fursa hii kuwaomba
wananchi kuwafichua maderva wanaokwenda mwendo kasi kupitia namba 08007575 ama
0715 009953 au 0658 376012.
Aidha niwatake madereva kuzingatia sheria za
usalama barabarani na kwa wale watakao kaidi Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani
hatutasita kuwachukulia hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengi.
Asanteni kwa kunisikiliza.
Imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Pwani
Kamishina Msaidizi Jafari Ibrahim.
|
No comments:
Post a Comment