Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi
Kida na Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo
(UNDP) Tanzania, (Ushauri na Miradi), Amon Manyama wakipitia makabrasha
ya mafunzo ya siku moja juu ya Uimarishaji wa Ushirika wa Akiba na
Mikopo kwa Viongozi wa Vyama vya Ushirika (SACCOS na VICOBA) na Maafisa
Ushirika wa kutoka Wilaya za Bunda, Bukoba na Sengerema yaliyoandaliwa
na ESRF na kufadhiliwa na Shirika la Maendeleo (UNDP) kabla ya kuwasili
mgeni rasmi kufungua mafunzo hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika
Hoteli ya Malaika Beach Resort jijini Mwanza.
Na Mwandishi Wetu, Mwanza
IMEELEZWA
kuwa matatizo ya uendeshaji wa vyama vya ushirika hasa ya
kutokuzingatiwa kwa sheria na kanuni za ushirika, wizi na ubadhirifu wa
mali yamedhoofisha sana ushirika Mkoani Mwanza.
Hayo
yamesema na Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo katika hotuba yake
iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya ya Ilemela, Manju Msambya
kwenye ufunguzi wa Mafunzo ya Uimarishaji wa Ushirika wa Akiba na
Mikopo, Mwanza.
Alisema
kutokana na ukweli huo ni vyema vyama vya ushirika vikawa makini katika
uchaguzi na kuhakikisha kwamba kila wanapofanya uchaguzi wanachagua
viongozi wazuri wenye uchungu na maendeleo ya ushirika na siyo
wanaotanguliza maslahi yao binafsi na kupuuza ya wengi.
“Tusaidiane kupambana na maovu na kujenga ushirika ulio imara.” Alisema.
Alisema pamoja na changamoto za kiuongozi Mwanza kwa sasa imepiga hatua kubwa upande wa SACCOS na VICOBA.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi
Kida akifurahi jambo na Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya Ilemela, Manju
Msambya aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kufungua mafunzo hayo
mara tu baada ya kuwasili ukumbini hapo.
“...
hatuna budi kuyalinda mafanikio haya kwa uwezo wetu wote. Mafanikio
hayo tutayalinda kwa kuhakikisha kuwa SACCOS zinaendeshwa kitaalamu na
kwamba sheria na kanuni za ushirika zinazingatiwa ipasavyo.” alisema
Aidha
Mkuu huyo wa mkoa, alishukuru ESRF na UNDP kwa kusaidia kugharamia
mafunzo kwa watendaji wa SACCOS ili waweze kufanyakazi zao kwa misingi
stahiki.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa masuala ya Kiuchumi na
Kijamii (ESRF), Dk Tausi Kida alisema lengo la mafunzo hayo ni
kuimarisha ushirika wa akiba na mikopo mkoani Mwanza.
Akizungumzia
historia ya mradi alisema wao kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo
la Umoja wa Mataifa (UNDP), Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa
(UNEP) pamoja Tume ya mipango, walianza kutekeleza mradi wa kukuza
uchumi, kuleta maendeleo endelevu kupitia utunzaji mazingira, usawa wa
kijinsia na kupunguza kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi
yaani (PEI) toka mwaka 2014.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi
Kida akitoa maelezo ya utangulizi juu ta madhumuni ya mafunzo hayo kwa
washiriki kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua rasmi.
Alisema
tafiti mbili chini ya mradi wa PEI zilizofanyika katika wilaya za
Bunda, Ileje, Sengerema, Bukoba vijijini, Ikungi na Nyasa kubaini
changamoto na fursa zinazopatikana katika wilaya hizo.
Alisema
matokeo ya tafiti yalionyesha umuhimu wa kuzipa uwezo taasisi za
kifedha kama SACCOSS, VICOBA na vikundi mbalimbali vya kifedha kwa
kuzijengea uwezo wa kitaaluma na kifedha.
Alisema
hata hivyo pamoja na matokeo hayo Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP) lilitenga na kutoa fungu la fedha na kuipatia benki ya
Twiga ili kukopesha kwa riba nafuu kwenye taasisi kama SACCOSS na VICOBA
kwa lengo kuu kuweza kuwafikia wananchi wengi zaidi ili waweze kupata
fursa ya kukuza mitaji yao na kuwafanya waweze kutekeleza fursa hizi
katika maeneo yao.
Wataalamu mbalimbali wakiwemo Dk. Jones Kaleshu kutoka Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi walishiriki kutoa mada.
Mgeni
rasmi Mkuu wa wilaya Ilemela, Manju Msambya akizungumza kwa niaba ya
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wakati akifungua rasmi mafunzo ya siku moja juu
ya Uimarishaji wa Ushirika wa Akiba na Mikopo kwa Viongozi wa Vyama vya
Ushirika (SACCOS na VICOBA) na Maafisa Ushirika wa kutoka Wilaya za
Bunda, Bukoba na Sengerema yaliyoandaliwa na ESRF na kufadhiliwa na
Shirika la Maendeleo (UNDP) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika
Hoteli ya Malaika Beach Resort jijini Mwanza.
Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya Ilemela, Manju Msambya akisisitiza jambo kwa washiriki (hawapo pichani).
Pichani
juu na chini ni baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Ushirika (SACCOS na
VICOBA) na Maafisa Ushirika wa kutoka Wilaya za Bunda, Bukoba na
Sengerema wakifuatilia kwa umakini hotuba ya mgeni rasmi (hayupo
pichani).
Mkurugenzi
Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) Tanzania,
(Ushauri na Miradi), Amon Manyama akitoa maelezo kuhusu mradi wa PEI na
salamu kutoka UNDP kwa washiriki wa mafunzo hayo.
Mkuu
wa Idara ya Maarifa na Mawasiliano wa ESRF ambaye pia ni Mratibu wa
mradi wa Kukuza Uchumi, Kuleta Maendeleo Endelevu Kupitia Utunzaji
Mazingira, Usawa wa Kijinsia na Kupunguza Mabadiliko ya Tabia Nchi,
Margareth Nzuki akitowasilisha matokeo ya Tafiti PEI 2014; Mchango wa
Huduma za Kifedha (Akiba na Mikopo) katika maendeleo ya jamii vijijini.
Mgeni
rasmi Mkuu wa wilaya Ilemela, Manju Msambya akinyanyua juu kitabu cha
"Mwongozo wa Mafunzo ya Uimarishaji wa Ushirika wa Akiba na Mikopo,
Elimu ya Ujasiriamali na Stadi za Biashara" kama ishara ya uzinduzi
rasmi wa mwongozo huo ulioandaliwa na ESRF. Wanaoshuhudia tukio hilo
ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii
(ESRF), Dk. Tausi Kida (kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) Tanzania, (Ushauri na Miradi), Amon
Manyama (kulia).
Mgeni
rasmi Mkuu wa wilaya Ilemela, Manju Msambya ( wa pili kushoto)
aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi
ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida
(kushoto), Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
Maendeleo (UNDP) Tanzania, (Ushauri na Miradi), Amon Manyama (wa pili
kulia) na Mkuu wa Idara ya Maarifa na Mawasiliano wa ESRF ambaye pia ni
Mratibu wa mradi wa Kukuza Uchumi, Kuleta Maendeleo Endelevu Kupitia
Utunzaji Mazingira, Usawa wa Kijinsia na Kupunguza Mabadiliko ya Tabia
Nchi, Margareth Nzuki kwa pamoja wakiwa wamenyanyua kitabu cha Mwongozo
wa Mafunzo ya Uimarishaji wa Ushirika wa Akiba na Mikopo, Elimu ya
Ujasiriamali na Stadi za Biashara mara baada ya kuzinduliwa na mgeni
rasmi kwenye mafunzo ya siku moja Juu ya Uimarishaji wa Ushirika wa
Akiba na Mikopo kwa Viongozi wa Vyama vya Ushirika (SACCOS na VICOBA) na
Maafisa Ushirika wa kutoka Wilaya za Bunda, Bukoba na Sengerema
yaliyoandaliwa na ESRF na kufadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la
Maendeleo (UNDP) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya
Malaika Beach Resort jijini Mwanza.
Lungu
Phares kutoka SELF Micro finance Fund akielezea shughuli mbalimbali
zinazofanywa taasisi ikiwemo utoaji mikopo wenye masharti nafuu.
Dkt.
Jones Kaleshu kutoka Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi akiwasilisha mada ya
hali ya Ushirika ya kuweka na kukopa nchini;changamoto na fursa
zilizopo katika mafunzo ya siku moja juu ya Uimarishaji wa Ushirika wa
Akiba na Mikopo kwa Viongozi wa Vyama vya Akiba na Mikopo pamoja na
Maafisa Ushirika wa Wilaya iliyoandaliwa na ESRF na kufadhiliwa na
Shirika la Maendeleo UNDP yaliyofanyika jijini Mwanza katika Hoteli ya
Malaika Beach Resort.
Baadhi ya washiriki wakijadiliana jambo wakati wa uwasilishaji wa mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye mafunzo hayo.
Afisa
Ushirika wa Bunda, Saulo Lunyeka akiwasilisha ya Utawala wa Majanga na
Usimamizi wa Akiba na Mikopona Umuhimu wake kwa wananchama wa jamii;
umuhimu wa kukuza mitaji.
Mgeni
rasmi Mkuu wa wilaya Ilemela, Manju Msambya aliyemwakilisha Mkuu wa
Mkoa wa Mwanza (wa nne kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (wa nne kulia),
Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP)
Tanzania, (Ushauri na Miradi), Amon Manyama (wa pili kushoto) pamoja
na Mkuu wa Idara ya Maarifa na Mawasiliano wa ESRF ambaye pia ni Mratibu
wa mradi wa Kukuza Uchumi, Kuleta Maendeleo Endelevu Kupitia Utunzaji
Mazingira, Usawa wa Kijinsia na Kupunguza Mabadiliko ya Tabia Nchi,
Margareth Nzuki (kushoto) katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo
ya siku moja juu ya Uimarishaji wa Ushirika wa Akiba na Mikopo kwa
Viongozi wa Vyama vya Akiba na Mikopo pamoja na Maafisa Ushirika wa
Wilaya yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.
Mgeni
rasmi Mkuu wa wilaya Ilemela, Manju Msambya aliyemwakilisha Mkuu wa
Mkoa wa Mwanza (wa nne kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (wa nne kulia),
Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Amon Manyama (wa
pili kushoto) pamoja na Mkuu wa Idara ya Maarifa na Mawasiliano wa ESRF
ambaye pia ni Mratibu wa mradi wa Kukuza Uchumi, Kuleta Maendeleo
Endelevu Kupitia Utunzaji Mazingira, Usawa wa Kijinsia na Kupunguza
Mabadiliko ya Tabia Nchi, Margareth Nzuki (kushoto) katika picha ya
pamoja na Wanawake Viongozi wa Vyama vya Akiba na Mikopo pamoja na
Maafisa Ushirika wa Wilaya.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
No comments:
Post a Comment