Viongozi wa
vyama vya siasa vitano wamevitaka Vyama
na asasi za kiraia kutoendelea kufanya tafiti na kuwapa asilimia
wagombea kiushabiki bila ya kufuata maadili na kanuni za kitafiti, ambayo
matokeo ya tafiti zao zimekuwa zikileta mtafaruku katika jamii kwa kueta za ama
kumdhoofisha mmoja kati ya wagombea waliotajwa katika tafiti husika.
SOMA TAMKO
ZIMA LA VIONGOZI WA VYAMA VITANO BAADA
YA KUKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI KUZUNGUMZIA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU.
Viongozi wa
vyama vya siasa vitano AFP, UMD, CHAHUSTA, JAHAZI ASILIA NA DEMOKRASIA MAKINI
kwa pamoja tumeungana kutoa wito kwa wanasiasa wenzetu, viongozi wa dini na
wananchi wote kwa jumla kuhusiana na uchaguzi huu unaotarajiwa kufanyika
ifikapo tarehe 25/10/2015.
Tamko hili
ni pamoja na:-
1. Tunawapongeza
wagombea wote wa nafasi ya Urais kwa kuendelea kufanya kampeni kwa njia ya
amani na Utulivu.
2.
Tunawataka watanzania wote waliojiandikisha kupiga kura wajitokeze kwa wingi
siku ya tarehe 25/10/2015 kupiga kura kwa kuchagua viongozi wanaowataka kwa amani
na Utulivu.
3. Viongozi
wa vyama vya siasa na wagombea wa nafasi mbalimbali, Urais, Ubunge na Madiwani
waache kutoa maneno ya kuwatia hofu wapiga kura kwamba tunaweza kuibiwa kura na
badala yake tuwahamasishe zaidi kujitokeza kwa wingii kupiga kura na kuiamini
tume ya taifa ya uchaguzi kuwa watatenda haki kwa wagombea wote bila kujali
hadhi ya chama cha siasa anachotoka mgombea.
4.Viongozi
wa dini wanaotaka kuwafanyia kampeni wagombea wasifanye hivyo katika nyumba za
ibaada na badala yake wakipenda kufany ahivo watumie majukwaa ya kisia sa na
sio madhabahu.
5.Viongozi
wa vyama vya siasa waache kutoa vitisho kwa wapiga kura kwa kuwatia hofu ya
kutabiri kuwepo kwa umwagikaji wa damu.
6.
Viongozi wa asasi za kiraia wasiendelee
kufanya tafiti na kuwapa asilimia wagombea kiushabiki bila ya kufuata maadili
na kanuni za kitafiti mabyo matokeo ya tafiti zao zimekuwa zikileta mtafaruku
katika jamii kwa kueta za ama kumdhoofisha mmoja kati ya wagombea waliotajwa
katika tafiti husika.
7. Mwisho
tunawataka watanzania wote kuwa makini na kuyadharau matamko yote yenye nia ya
kuwatia hofu na kuendelea kuipenda nchi yetu ya Aamini na Utulivu katika
kipindi hiki cha uchaguzi mkuu wa Taifa letu.
Na vilevile viongozi wa dini
waendelee kuliombea taifa letu libaki kuwa na utulivu wakati wote wa uwepo wetu
katika nchi yetu.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
Friday, October 02, 2015
Home
SIASA
UTAFITI KWA WAGOMBEA:- Lisome tamko la Viongozi wa Vyama vitano vya siasa kuelekea Uchaguzi mkuu October 25,2015.
UTAFITI KWA WAGOMBEA:- Lisome tamko la Viongozi wa Vyama vitano vya siasa kuelekea Uchaguzi mkuu October 25,2015.
Tags
# SIASA
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
SIASA
Labels:
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment