Aliyekuwa
mgombea ubunge wa jimbo la Kahama, Bw.James Lembeli ameelezea kinachoendelea
katika maisha yake ya kisiasa hasa baada ya kushindwa katika uchaguzi wa mwaka
huu akiwa ndani ya chama chake kipya cha CHADEMA.
Akiongea
katika taarifa rasmi kwa wananchi wa jimbo Kahama, Lembeli amesema kuwa hivi sasa
atajikita zaidi katika shughuli za chama chake pamoja na shughuli alizokuwa
akizifanya kabla ya kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Alisema kuwa
ataendelea kufanya kazi zake na mashirika ya kimataifa kama mjumbe wa Bodi
mbalimbali. Pia, ataendelea kufanya kazi ya kusimamia radio yake (Kahama FM)
ambayo amedai kuwa taarifa zilizosambazwa kuwa ameiuza kulipa deni la mkopo
aliopewa kuendesha kampeni sio za kweli.
Pia, Lembeli
amewashukuru wananchi waliojitokeza kumuunga mkono na kuahidi kuendelea
kushirikiana nao katika masuala ya maendeleo na ataendeelea kushirikiana nao
kukamilisha miradi mbalimbali aliyokuwa ameanza kuitekeleza kwa juhudi zake
binafsi.
Kadhalika,
Lembeli amekanusha taarifa zilizokuwa zimesambazwa kuwa alikamatwa na jeshi la
polisi mara tu baada ya Jumanne Kishimba wa CCM kutangazwa kuwa mshindi.
Kuhusu afya
yake, alisema kuwa yeye ni mzima tofauti na habari zinazoendelea kuenea kuwa ni
mgonjwa hasa baada ya kupata ajali ya gari na matokeo kutangazwa.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment