EPL 2015 / 2016:-Matokeo ya mechi za October 4,2015 za Ligi Kuu Uingereza. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, October 05, 2015

EPL 2015 / 2016:-Matokeo ya mechi za October 4,2015 za Ligi Kuu Uingereza.

Arsenal, wakicheza kwao Emirates, walianza Mechi hii ya Ligi Kuu Uingereza msimu huu 2015/2016 vizuri mno na kufanikiwa kuifunga Manchester United Bao 3 ndani ya Dakika 19 za kwanza.

Arsenal walipata Bao la kwanza katika Dakika ya 6 alilofunga Alexis Sanchez na Dakika 1 baadae Mesut Ozil alipiga Bao la pili na kisha Sanchez kufunga Bao la 3 katika Dakika ya 19.
Matokeo haya yamewafanya Arsenal wakamate Nafasi ya Pili kwenye Ligi kuu wakiwa Pointi sawa na Man United lakini wao wana ubora wa Magoli na wote wako nyuma ya Vinara Man City ambao wana Pointi 16, Pointi 2 mbele ya Arsenal na Man United.


Ligi Kuu England sasa itakaa pembeni kupisha Mechi za Kimataifa na kurejea tena dimbani Oktoba 17,2015.

Jumamosi Oktoba 17,2015.

1445 Tottenham v Liverpool          

1700 Chelsea v Aston Villa             

1700 Crystal Palace v West Ham             

1700 Everton v Man United               

1700 Man City v Bournemouth                

1700 Southampton v Leicester                

1700 West Brom v Sunderland                

1930 Watford v Arsenal        

Jumapili Oktoba 18,2015

1800 Newcastle v Norwich             

Jumatatu Oktoba 19,2015

2200 Swansea v Stoke

LIGI KUU UINGEREZA 2015/2016 -  MATOKEO.

Everton 1 – 1 Liverpool    

Arsenal 3 – 0 Man United           

Swansea 2 – 2 Tottenham 

Liverpool imemfukuza kazi Meneja wao Brendan Rodgers kuanzia Jana October 04,2015 mara tu baada ya kutoka Sare 1-1 na Everton kwenye Dabi ya Merseyside ya Mahasimu hao wa Jiji la Liverpool.

Matokeo haya ya yameiacha Liverpool ikiwa Nafasi ya 10 kwenye Ligi Kuu Uingereza ikiwa Pointi 6 nyuma ya Vinara wa Ligi Man City.

Uamuzi huu wa umethibitishwa na Klabu ya Liverpool ambayo imetoa tamko kuwa wameanza kusaka Meneja mpya lakini tetesi ni kuwa Carlo Ancelotti, Frank de Boer na Jurgen Klopp wamehusishwa na kazi hiyo.

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.  


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad