![]() |
Wagombea nafasi ya urais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na
Edward Lowassa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Zimebaki siku 45 kuanzia leo kabla
ya kufikiwa siku ya kupiga kura Oktoba 25 mwaka huu,2015 -Uchunguzi uliofanywa
na Nipashe umebaini kuwa mikoa hiyo tisa, ikiwamo yenye majiji makubwa ya Dar es Salaam, Mwanza na Mbeya, ndiyo
yenye watu wengi zaidi waliojiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura
kwa kutumia mfumo wa Kielektroniki (BVR).
Takwimu zilizokusanywa na Nipashe
kwa siku kadhaa kutoka katika ofisi za waratibu wa uchaguzi wa mikoa mbalimbali
nchini zinaonyesha kuwa kwa ujumla, mikoa hiyo tisa ina jeuri ya kutoa rais
ajaye kwani ina mtaji wa kura zinazozidi asilimia 50.
Taarifa za Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC) zinaonyesha kuwa hadi kufikia Julai 30, 2015 na hata baada ya kuongezwa
siku nyingine nne katika wiki ya kwanza ya Agosti, 2015 ili kukamilisha kazi ya
uandikishaji kwa kutumia BVR, idadi ya Watanzania waliojiandikisha
ilifikia 23,782,558, sawa na asilimia 99.5 ya matarajio.
Kati ya hao, Nipashe imebaini kuwa
watu 12,119,263 wanatoka katika mikoa tisa inayoongozwa na Dar es Salaam,
Mwanza na Mbeya; na ambayo kimahesabu ni sawa na asilimia 50.96 ya watu wote
waliojiandikisha.
Mbali na Dar es Salaam, Mwanza na
Mbeya, mikoa mingine kati ya tisa iliyo na mtaji mkubwa wa kura zinazotosha
kutoa mshindi wa urais Oktoba 25 ni Tanga, Arusha, Morogoro, Tabora, Dodoma na
Kagera.
Dk. Magufuli wa CCM na Lowassa wa
Chadema anayewakilisha pia muungano wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) vya NCCR-Mageuzi, NLD na Chama cha Wananchi (CUF), wanachuana
pia na Fahmy Dovutwa wa UPDP, Hashim Rungwe wa Chama cha Umma (Chauma),
Maximillian Lymo wa TLP, Anna Mghwira wa ACT-Wazalendo, Chief Lutasola Yemba wa
ADC na Janken Kasambala wa NRA.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya Mwaka 1977, Ibara ya 41 (6), inaeleza kuwa mgombea yeyote wa nafasi
ya urais atakayepata kura nyingi dhidi ya wagombea wengine ndiye
atakayetangazwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, Sheria ya
Taifa ya Uchaguzi ya Mwaka 1985 (Sura ya 343), vifungu vya 35E na 35F inatoa
mamlaka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kumtangaza mgombea
aliyepata kura nyingi kuwa mshindi wa nafasi ya urais.
Kwa sababu hiyo, mgombea yeyote
atakayefanikiwa kupata asilimia 100 ya kura katika mikoa hiyo tisa
atajihakikishia kuwa rais ajaye kwa ushindi wa zaidi ya asilimia 50, hata kama
atapata kura za idadi ndogo katika maeneo mengine ya nchi.SOMA ZAIDI UTAFITI HUU KWA KUBOFYA HAPA.
|
Post Top Ad
Friday, September 11, 2015

UCHAGUZI MKUU 2015-TANZANIA:-Kura za ushindi Urais hizi hapa.
Tags
# DONDOO
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
Makala Inayofuata
HISTORIA:-Mjue Mufti mpya wa Tanzania.
Makala Iliyopita
KAMPENI UBUNGE NGARA 2015:-Matukio tofauti ya mikutano ya Dr Petter Bujari mgombea CHADEMA.
Muonekano wa Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
AnonymousDec 10, 2019Viongozi Wilayani Kasulu watakiwa Kuimarisha Usalama Katika Korongo la Bolelo.
AnonymousJun 29, 2019Shirika la Ndege la Tanzania Laanza Safari za Afrika Kusini Leo 28/06/2019.
AnonymousJun 28, 2019
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment