TAARIFA:-CHADEMA tawi la MAREKANI yakanusha Taarifa kuhusu kuwapokea Dr Wilbroad Slaa na Mheshimiwa Freeman Mbowe. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, September 20, 2015

TAARIFA:-CHADEMA tawi la MAREKANI yakanusha Taarifa kuhusu kuwapokea Dr Wilbroad Slaa na Mheshimiwa Freeman Mbowe.


Mwenyeketi wa Tawi la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Washington DC, Kalley Pandukizi  (kulia) akiwa na Katibu wa chama hicho, Ndugu Libe Mwang'ombe (katikati) alipotoa kadi rasmi kwa Beautician maarufu na designer Mtanzania, Linda Bezuidenhout (kushoto). Picha ya Maktaba.

 Napenda kuchukua nafasi hii kukanusha taarifa ya uongo na uzushi iliyoenezwa kupitia mitandao ya kijamii , tarehe 18 Septemba 2015 iliyoanzia kwenye JamiiForums yenye kichwa cha habari “Mbowe asalimu amri kwa Dr Slaa”.

 Katika taarifa hiyo mwandishi amenitaja mimi Kalley Pandukizi kama mmoja wa viongozi wa CHADEMA tawi la DMV pamoja na viongozi wenzangu kuwa tumewapokea viongozi hao wa juu hapa Marekani na wapo katika hoteli moja Ohio kwa ajili ya mazungumzo binafsi.

Napenda kueleza umma kuwa taarifa hii si ya kweli, ni ya uongo na uzushi yenye lengo la kuhadaa umma wa Watanzania kuwa kuna mazungumzo kati ya viongozi hawa hapa Marekani. Pia ina lengo la kunichafulia jina mimi kama Mwenyekiti wa CHADEMA tawi la DMV.

Mwisho napenda kutoa wito kwa wanachama na wapenzi wa CHADEMA pamoja na UKAWA kwa ujumla wake, kupuuzia taarifa kama hizi zenye lengo la kupotosha na kuhadaa umma kwa malengo mabaya ya kisiasa, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25.

Imetolewa na:-

Mwenyekiti wa CHADEMA - DMV, Marekani

Kalley Ammy Pandukizi


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad