FAIDA YA TUNDA LA
PARACHICHI - PEA (AVOCADO)
Ndani ya tunda hili kuna maji kiasi kidogo sana ukilinganisha na matunda
mengine lakini kuna mafuta mengi na unaweza kuchanganya kula na tunda lingine
kama vile apple, ndizi, chungwa au hata maziwa kwa kutengeneza juisi.
TINDIKALI
Licha ya kuwa na mafuta parachichi lina tindikali (acid) mbalimbali ikiwemo
inayojulikana kama amino ambayo husaidia sana kukinga na kutibu maradhi katika
mwili wa binadamu. Tunda hili pia lina protini ya kiwango cha juu.
Pia kuna tindikali inayoitwa oleic acid kwenye parachichi ambayo husaidia
kukinga magonjwa ya moyo, kiharusi na kansa.
VITAMINI “E” NA B6
Imeelezwa na wataalamu kuwa tunda hili lina kiwango kikubwa cha vitamini E
kuliko ile inayopatikana kutoka kwenye mazao ya wanyama.Parachichi lina
vitamini hiyo nyingi kuliko inayopatikana katika mayai ambayo yanasifika kwa
kuwa na vitamini e, hivyo hii inathibitisha kuwa lina faida kubwa mwilini.
Licha ya vitamini E pia ndani ya parachichi kuna vitamini B6 na kuna madini ya
chuma (Iron) kwa wingi na madini ya potassium, pamoja na vitamin B6 na E mlaji
anaweza kuletawa nafuu sana kama alikuwa na matatizo ya stress, matatizo ya
uzazi kama ugumba na jogoo kutopanda mtungi Nguvu za kiume pia tunda hili
linasaidia (impotence) .
FAIDA ZA PARACHICHI
Licha ya binadamu kufaidika na virutubisho vya tunda hili kuna faida nyingi za
parachichi kama vile majani ya mti wake pamoja na magamba, baadhi ya watu
hutumia kutibu maradhi ya kuharisha.
Majani na magamba hayo hutibu pia tatizo la gesi tumboni, kutuliza kikohozi
pamoja na matatizo ya ini na kusafisha njia ya mkojo.
Hata hivyo, kwa mujibu wa wataalamu wa dawa za mitishamba, dawa hii haifai
kutumiwa na wanawake ambao wana mimba kwani wakitumia inaweza kusababisha
kuharibika kwa ujauzito.
HEDHI
Hata hivyo, wataalamu wa tiba mbadala wanasema dawa hiyo inaweza kuwasaidia
sana wanawake ambao wameshindwa kuona siku zao kwa wakati, na wakitumia vyema
wanaweza kuanza kuona siku zao.
Aidha, tunda hili linasaidia uyeyushaji wa chakula tumboni hasa kwa wale wenye
matatizo ya vidonda vya tumbo, kwani parachichi lina nyuzinyuzi “fiber” ambayo
ni muhimu kukinga kuta za utumbo. Watu wenye maradhi ya anaemia, diabetes,
matatizo ya mfumo wa neva, matatizo ya mishipa ya moyo hasa wa artery
wanashauriwa kula tunda hili mara nyingi.
Lakini pia tunda hili limethibitishwa na wataalamu kuwa linapunguza kwa kiwango
kikubwa cholesterol kutoka kwenye damu hasa kwa watu wanene.
Tunda hili husaidia kulainisha ngozi na kuondoa mikunjo, hung`arisha na
kulainisha nywele na kuzisaidia kukua pia kuziimarisha na kuzuia kukatikakatika.
Parachichi unaweza kulila kwa kulimenya au kwa kulisaga na kutengeneza juisi na
kama nilivyoeleza hapo juu unaweza kuchanganya na matunda mengine kama
tulivyoyataja na hutaharibu virutubisho vilivyomo badala yake utaongeza ubora
wa juisi yako.
Watoto wadogo pia unaweza kuwapa tunda hili na wakafaidika na haya
tuliyoyaandika.
Parachichi pia huweza kutumika kama siagi kwa kupaka kwenye mkate au
kuchanganya na wali.
Haya wale wanaopenda ngozi zao za mwilini zisijikunje hata wakiwa watu wazima
wadumu kula tunda hili kila siku katika maisha yao basi ngozi za mwili wao
hazitajikunja hata usoni watakuwa kila siku vijana hata wakiwa wazee.
KATIKA TENDO LA NDOA
husaidia katika uzalishaji wa mbegu maana tunda linamafuta mafuta yakutosha na
hii husababisha stimulation ya hormones wakati watendo la ndoa
na pia juice yake huwasaidia wote wanawake na wanaume katika tendo landoa kua
na nguvu kwamda mrefu bila kuchoka na hii kuongeza ufanisi katika tendo hilooo.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo
na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia
tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment