Majengo
pacha ya ghorofa 35 ya PSPF TOWERS mtaa wa Sokoine jijini Dar es salaam
yaliyozindulia Jana Septemba 16, 2015 na Rais wa Tanzania Dr.Jakaya Mrisho Kikwete.
|
Kudumu kwa rekodi ya urefu ya PSPF Towers lenye minara miwili na ukubwa wa mita za mraba 73,000, kutategemea kukamilika kwa majengo mengine yanayochipua kwa kasi katika Afrika. |
Rais Kikwete
akifunua pazia kuzindua rasmi majengo pacha ya PSPF TOWERS hapo jana September 16,2015.
|
Rais Kikwete
akikata utepe kuzindua rasmi majengo pacha ya PSPF TOWERS… PICHA NA IKULU.
PSPF Towers
ni moja ya majengo machache marefu barani Afrika na ndiyo jengo refu zaidi
lililokamilika Afrika Mashariki na Kati, likiwa na urefu wa mita 147.
Majengo
mengine marefu Afrika ni Carlton Centre (mita 223) lililopo Afrika Kusini,
Hassan II Mosque (mita 210) lililopo Moroko, Ponte City (mita 173) lililopo
Afrika Kusini, Necon House (Mita 160) lililopo Nigeria, Marble Tower (mita
152), Pear dawn (mita 152), Pear dawn (mita 152), Met Life Centre (mita 150) na
88 on field (mita 147) yote ya Afrika ya kusini.
Jengo hilo
lililozinduliwa na Rais wa Tanzania ,Dr. Jakaya Kikwete,jana September 16,2015 ujenzi wake ulitumia miaka
minne tangu mwaka 2011 hadi 2015 limegharimu shilingi bilioni 139.20 za
Tanzania lina maeneo ya ofisi na nyumba za makazi 88. Pia katika jengo hili
kuna sehemu ya mgahawa, mabenki, bwawa la kuogelea, Sehemu za kufanyia mazoezi,
maegesho ya magari na sehemu nyingine muhimu....Habari kwa hisani ya BBC SWAHILI.
|
No comments:
Post a Comment