Meza kuu
katika warsha ya wadau wa ajira kwa vijana iliyofadhiliwa na Mpango wa Shirika
la Utafiti wa Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada (IDRC) na kuratibiwa na
ESRF.
Kutoka kushoto ni Afisa kutoka Wizara ya Kazi na Ajira kitengo cha Ajira,
Joseph Nganga, Mkurugenzi wa Kazi katika Wizara ya Kazi na Ajira,
Ally M. Ahmed, Mkuu wa utafiti na machapisho Taasisi ya Utafiti wa
Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene, Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel na
Mratibu Kazi wa Shirika la Kimataifa la Kazi (ILO) Dk. Annmarie Kiaga… (Picha zote na Zainul Mzige
wa Modewjiblog).
Na Mwandishi
wetu
PAMOJA na
kuwepo na maendeleo ya kuridhisha katika suala la ajira kwa vijana, serikali
imekiri kwamba ukosefu wa ajira bado ni tatizo kubwa duniani na kwa taifa kwa
ujumla.
Kutokana na
hali hiyo suala la ajira kwa vijana limebaki kuwa ajenda kuu nchini.
Kauli hiyo
imetolewa na Mkurugenzi wa Kazi katika Wizara ya kazi Ally M. Ahmed wakati akifungua warsha ya siku
moja ya wadau wa ajira kwa vijana iliyofanyika hoteli ya Double Tree by Hilton.
Alifanya
ufunguzi huo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eric Shitindi.
Alisema
Tanzania inaendelea kukabiliana na tatizo la ajira kutokana na wigo mdogo wa
fursa za ajira, tatizo la utaalamu na ukosefu wa uzoefu .
Alisema hata
hivyo vijana wanaoamua kujiajiri wenyewe wamekuwa wakikabiliana na tatizo kubwa
la mtaji, maeneo ya kufanyia kazi na utaalamu katika ujasiriamali
utakaowawezesha kuendesha miradi wanayoibuni.
Alisema
kutokana na uwapo wa sera, mipango na miradi ya maendeleo kuhusu ajira kwa
vijana inayoendeshwa kitaifa na kimataifa kumekuwepo na dalili njema za
kupungua kwa ukosefu wa ajira.
Alisema
utafiti wa mwaka 2014 (ILFS) umeonesha kwamba ukosefu wa ajira umepungua kutoka
asilimia 11.7 kwa mwaka 2006 hadi kufikia asilimia 10.3 ka mwaka 2014 huku kwa
vijana (wenye umri wa miaka 15 hadi 35) ukipungua kutoka asilimia 13.2 kwa
mwaka 2006 hadi asilimia 11.7 kwa mwaka 2014.
|
Mkuu wa
Utafiti na mchapishi wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF),
Profesa Fortunata Makene akitoa hotuba ya utangulizi katika warsha ya vijana na
ajira iliyofanyika hoteli ya Double Tree by Hilton.
Katika hotuba yake ya
ufunguzi alitoa wito wa washiriki kuangalia kwa undani tatizo la ajira kwa
vijana na kutoa mwelekeo utakaosaidia watunga sera kuwa na sera madhubuti
kuhusu ajira kwa vijana.
Alisema
mafanikio yaliyopatikana hayaondoi ukweli kuwa kuna tatizo kubwa la ajira
miongoni mwa vijana na kutokana na mazingira ya sasa ni vyema wadau wa ajira
kuangalia kwa undani tatizo la ajira la sasa ili kutoa ushauri wa kukabiliana
nalo kwa kipindi kifupi na kirefu.
Shitindi
alisema kwamba serikali inafurahishwa na juhudi zinazofanywa na wadau
mbalimbali kutafuta majibu ya tatizo la ajira, majibu ambayo alisema yakifanywa
vyema yatasaidia sana wataalamu wa serikali kutengeneza sera na kanuni zitakazo
kidhi haja.
Alisema ipo
haja kwa wachambuzi (watafiti) kuelekeza nguvu zao katika kutafiti soko la
ajira ili kusaidia watengeneza sera kuona mahitaji ya soko katika miaka kadhaa
ijayo.
Alisema
wakati uchumi wa Tanzania unakua kwa asilimia 7 kwa mwaka kwa miaka kumi
iliyopita ajira zimekuwa haziendi sambamba na ukuaji wa uchumi na hivyo kuleta
maswali mengi ya sintofahamu.
Alisema
serikali kwa sasa inataka kuhakikisha kwamba inaboresha upatikanaji wa ajira
lakini hilo linawezekana kama taasisi zake zinazotengeneza sera na kuweka
mipango zinatambua tatizo na kuona namna ya kuliangalia.
Alisema
watafiti wana wajibu mkubwa wa kusaidia serikali kuwezesha vijana kuwa na kazi
zenye staha kama sera ya ajira ya taifa inavyotaka.
|
Mkurugenzi
wa kazi wizara ya kazi na ajira, Ally Msaki Ahmed, akisoma hotuba kwa niaba ya
Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na Ajira, Eric Shitindi katika warsha ya kitaifa ya
ajira kwa vijana iliyofanyika hoteli ya Duble Tree by Hilton. Katika hotuba
yake aliwataka washiriki kujadili kwa makini matatizo ya vijana na kutoa suluhu
itakayosaidia watendaji kutunga sera na kutoa mwelekeo mpya wa kukabiliana na
tatizo hilo.
Alisema kwa
kuangalia ukuaji wa kisekta, sekta ambayo sasa hivi inahitaji watu ndio ambayo
haina wataalamu wa kutosha na hivyo ukuaji wa sekta hizo kama za mawasiliano
hauendi sanjari na utaalamu uliopo katika soko.
Katibu Mkuu
huyo alitoa wito kwa watu binafsi na serikali kuhakikisha kwamba wanakabiliana
na vikwazo vya ajira kwa kutoa elimu na taaluma ili fursa zionekane na kutumika
ipasavyo.
Alisema tija
inaweza kuonekana katika ukubwa wa utaalamu, ubunifu na namna mafunzo
yanavyowawezesha wanafunzi kuwa na uhakika na kazi wanazotaka.
Alisema ipo
haja kwa wadau mbalimbali kushirikiana na serikali katika kuhakikisha kwamba vijana
wanaingizwa katika soko la ajira na tatizo la ajira linapunguzwa.
|
Kiongozi
Mpango wa ukuaji na ajira wa taasisi hiyo, Shirika la Utafiti ya Maendeleo ya
Kimataifa kutoka Canada (IDRC), Dk. Arjan de Haan akielezea sababu za taasisi hiyo kuunga mkono
tafiti kwa ajili ya kusaidia kupatikana ufumbuzi wa tatizo la ajira katika
warsha ya ajira na vijana iliyofanyika Double Tree by Hilton hotel.
Katika moja
ya maazimio yaliyotolewa na washiriki vijana, walitaka kuwepo na mabadiliko
makubwa katika utoaji elimu, ambapo walisema elimu itolewe kwa Kiswahili lakini
pia wanafunzi waandaliwe kuwa wabunifu na kujiajiri.
Aidha
wametaka kurejeshwa kwa shule za ufundi na shule maalumu kama ilivyokuwa
zamani.
Walisema
vijana Wanatakiwa kushiriki katika utengenezaji wa sera na kanuni na si
kushirikishwa na kutaka matakwa yao yanastahili kuangaliwa na kuzingatiwa ili
mtu ajifunze kila anachoona anaweza kukifanya vyema.
Warsha hiyo
ya ajira kwa vijana imewezeshwa na IDRC na kuratibiwa na ESRF na mada
mbalimbali ziliwasilishwa ambazo zilichambua masuala ya elimu, elimu ya ufundi,
changamoto na fursa za vijana katika ajira.
Aidha
kulikuwa na mada za majukumu ya serikali na sera katika kuboresha mchakato wa
ajira kwa vijana.
|
Mchumi na
Mshauri huru Bi. Mahjabeen Haji akiwasilisha mada kuhusu hali ya ajira kwa
vijana nchini katika warsha ya vijana na ajira ilyofanyika hoteli ya Double
Tree by Hilton, katika mada yake alielezea mazingira ya ajira ambapo elimu
katika sekta zinazokua kwa kasi kama Tehama ni kikwazo kikubwa katika kuwezesha
ajira kwa vijana.
|
Mkurugenzi
wa Salama Foundation, Shadrack John Msuya akiwasilisha mapendekezo ya vijana
juu ya namna ambavyo vipaji, elimu na ubunifu vinavyoweza kutengeneza ajira
kwenye maeneo ya Sayansi, Teknolojia, Kilimo na Ufugaji.Moja ya azimio ni kuwa
na sera mpya ya vijana yenye mpango
mkakati na tafiti zinazotekelezeka katika warsha ya vijana na ajira.
|
Mshauri
mwelekezi katika uanzishwaji na uendelevu wa biashara na maendeleo ya jamii,
Gidufana Gafufen akiwasilisha mapendekezo yaliyowasilishwa katika vikundi nini
kifanyike ili vijana wapende kilimo katika warsha ya vijana na ajira
iliyofanyika katika hoteli ya Double Tree by Hilton.
|
Pichani juu
na chini ni sehemu ya wadau pamoja na makundi ya vijana waliohudhuria warsha ya
wadau wa ajira kwa vijana iliyofadhiliwa na Mpango wa Shirika la Utafiti wa
Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada (IDRC) na kuratibiwa na ESRF.
|
Mmoja wa
washiriki akitoa maoni kwenye warsha ya wadau wa ajira kwa vijana
iliyofadhiliwa na Mpango wa Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Kimataifa kutoka
Canada (IDRC) na kuratibiwa na ESRF.
|
Picha
ya pamoja ya washiriki wa warsha ya
wadau wa ajira kwa vijana iliyofadhiliwa na Mpango wa Shirika la Utafiti wa
Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada (IDRC) na kuratibiwa na ESRF.
|
Mratibu Kazi
wa Shirika la Kimataifa la Kazi (ILO) Dk. Annmarie Kiaga (kulia) akiteta jambo
na baadhi ya washiriki.
|
Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel (kushoto) akifurahi jambo na Mtafiti Mwandamizi ESRF, Dk. Georgina Ole
Saibul mara baada ya kumalizika kwa warsha hiyo.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo
na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia
tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment