Kutokana
na ukubwa wa Tukio la Uchaguzi Mkuu wa Madiwani,
Wabunge na Rais wa
Jamhuri ya Muungano Tanzania siku ya Jumapili October 25 2015, stori zinazohusu Siasa zinakuja kila siku kwenye Headlines
na kila kubwa ambayo inanifikia nahakikisha tu na wewe inakufikia wakati
huohuo.
Imenifikia Taarifa kutoka Makao Makuu ya CCM,
Mtaa wa Lumumba Dar es Salaam ambapo January Makamba, Mjumbe wa Kamati ya Kampeni CCM ameitoa
Taarifa hii. Habari kwa hisani ya MILLARDAYO
|
Kwenye
kile alichokisema kuna hili jibu kuhusu Mgombea Urais kwenye Uchaguzi Mkuu 2015
anayewakilisha CCM, Dk. Magufuli kushiriki Midahalo
>>> ‘CCM ilipokea
mwaliko wa MCT na kuijibu tarehe 13 Septemba 2015.. CCM ilitoa kauli rasmi,
iliyosainiwa, ikithibitisha kushiriki mdahalo, tunaamini ni vyema mdahalo huu
ukaandaliwa na ushirika wa Taasisi mbalimbali zenye nia ya kuandaa… Magufuli
amekubali kushiriki Mdahalo wa Wagombea Urais‘ >>>- January Makamba.
|
Jana September 22,2015, kulikuwa na stori ambayo iligusa sana kwenye Siasa TANZANIA,
ishu ni Matokeo ya Utafiti uliofanywa na Taasisi ya TWAWEZA >>> ‘CCM
haikushangazwa na matokeo ya Utafiti wa TWAWEZA ambayo yanatoa ushindi wa 65%
kwa Ndugu John Magufuli dhidi ya 25% za Mgombea wa UKAWA… Matokeo ya Utafiti
huu ni ishara kwamba Watanzania wamemkubali na kumuelewa Ndugu Magufuli‘ >>> January Makamba.
|
Maneno mengine ya January Makamba haya hapa
>>> ‘Mwezi Agosti
2010 Taasisi ya SYNOVATE ilitoa Utafiti ikionesha CCM itashinda Uchaguzi wa
2010 kwa 61%, Wapinzani waliwalaani na kuwashitaki SYNOVATE… Kwenye Matokeo
halisi CCM ilipata Kura zilezile 61%‘
>>>- January Makamba.
Taarifa
yote ninayo hapa pia kama unahitaji kuisoma mwanzo mpaka mwisho.
|
No comments:
Post a Comment