![]() |
CHAMA cha ACT – Wazalendo kimesema
hadi sasa wamejitokeza wagombea katika majimbo 203 ya uchaguzi nchini huku kura
za maoni za kupata wagombea katika majimbo mbalimbali zikiendelea.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa chama
hicho, Samson Mwigamba, hadi kufikia Ijumaa iliyopita, chama hicho cha upinzani
nchini kilikuwa na wagombea 298 katika majimbo 203 nchini kati ya majimbo 265
yaliyopo.
Mwigamba aliuambia mtandao huu
kuwa chama hicho ambacho Kiongozi Mkuu wake ni aliyewahi kuwa Mbunge wa Kigoma
Kaskazini kupitia Chadema, Zitto Kabwe, kitasimamisha mgombea kwa kila jimbo la
uchaguzi nchini.
“Chama chetu kitasimamisha mgombea
katika kila jimbo nchini.Na hadi kufikia Ijumaa iliyopita, tulikuwa na wagombea
298 katika majimbo 203. Kwa sasa kura za maoni zinaendelea katika sehemu
mbalimbali nchini na baadhi yao wamekwisha kamilisha uteuzi wa wagombea,” alisema Mwigamba.
Alitaja baadhi ya majimbo yaliyopata
wagombea kuwa ni Kigoma Mjini ambako ameshinda Zitto, Kasulu Mjini alikoshinda
aliyekuwa Mbunge kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, Moses Machali na Kasulu Vijijini
ambako ameshinda Thomas Matatizo ambaye ni mwanasheria wa chama hicho.
Alisema majimbo mengine yalitarajiwa
kufanya kura za maoni jana ikiwamo Singida Mjini ambako anagombea Mwenyekiti wa
Taifa wa ACT – Wazalendo, Anna Mghwira, huku majimbo mengine yakitarajiwa
kufanya leo na kesho ikiwamo Ubungo ambalo litafanya kesho na ambako Mwigamba
amejitosa kuwania uteuzi huo.
“Majimbo mengine yanaendelea na kura
za maoni kwa sasa. Kwa mfano, Tarime Mjini, Tarime Vijijini, Bukombe, Singida
Mjini yanatarajiwa kufanya kura hizo kati ya leo (jana) na kesho (leo). Geita
Mjini walifanya, lakini kulitokea ukiukwaji wa taratibu na wakaomba zoezi hilo
lilirudiwe,” alieleza Mwigamba.
Aidha, alisema wanaendelea kupokea
baadhi ya wanachama waliokuwa katika vyama vingine vya upinzani ambao
wanajiunga na chama hicho, akitaja baadhi yao kuwa walikuwa wagombea katika
majimbo ya Musoma Mjini, Bunda Mjini, Tarime Mjini (wote wametoka Chadema) na
Mtama (ametoka CCM).
Kuhusu wagombea wa urais, alisema
hadi sasa amejitokeza mgombea mmoja, ingawa wapo wanawake wawili walioonesha
nia lakini hawajachukua fomu ambazo zitatolewa mpaka Agosti 11, mwaka huu.
Katibu Mkuu huyo wa ACT – Wazalendo
alisema vikao vya uteuzi vitaanza Agosti 12 kwa kukutana na Sekretarieti
itakayofuatiwa na Kamati Kuu Agosti 14, Halmashauri Kuu ya Taifa Agosti 15 na
Mkutano Mkuu utafanyika Agosti 16, mwaka huu kupitisha Mgombea wa Urais na
kufanyia marekebisho Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho.
ACT - Wazalendo ilipata usajili wake
wa kudumu Mei, 2014, na mapema mwaka huu, Zitto alijiunga nacho na kutangazwa
kuwa Kiongozi Mkuu. Ni chama kinachoamini katika misingi ya Ujamaa Demokrasia.
Source:-Mpekuzi blog
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
Friday, August 07, 2015

Home
SIASA
UCHAGUZI MKUU TANZANIA 2015:- Chama cha ACT-Wazalendo chatarajia kusimamisha wagombea hawa Katika Majimbo 203.
UCHAGUZI MKUU TANZANIA 2015:- Chama cha ACT-Wazalendo chatarajia kusimamisha wagombea hawa Katika Majimbo 203.
Tags
# SIASA
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
SIASA
Labels:
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment