MBIO ZA URAIS 2015 TANZANIA:- Hatimaye mgombea urais ADC achukua fomu Tume ya Uchaguzi NEC-Leo August 7, 2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, August 07, 2015

MBIO ZA URAIS 2015 TANZANIA:- Hatimaye mgombea urais ADC achukua fomu Tume ya Uchaguzi NEC-Leo August 7, 2015.

Mgombea urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Alliance for democratic Change ADC CHIEF LUTASOLA YEMBA  muda huu amechukua Form yake ya kuwania urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania huku akisindikizwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho form zinazotolewa na tume ya Taifa ya uchaguzi.Pichani ni mgombea huyo akiwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho akiwemo Mgombea mwenza SAID MIRAJI,pamoja na mlezi wa chama hicho HAMAD RASHID.
CHIEF LUTASOLA YEMBA akizngumza na wanahabari mbalimbali waliojitokeza katika makao makuu ya Tume ya taifa ya uchaguzi kushugudia tukio hilo ambapo akiangumza na wahabarai hao amesema kuwa ni hakika kuwa sasa tanzania inahitaji kiongozi anayeweza kuyafikia matatizo halisi ya mtanzania na kiongiozi ambaye ana nia ya dhati ya kuwasaidia watanzania jambo ambalo amesema kuwa kama watanzania watamwamini na kumpa nafasi ya kuiongoza Tanzania atahakikisha kuwa atawatumikia watanzania kwa uwezo wake wote.
SAID MIRAJ ni mgombea mweza wa nafasi ya urais wa jamhuri ya muungano wa tanzania ambapo akizngumza na wanahabari amesema nchini tanzania sasa upinzani wa kweli haupo kilichobali ni kuwatania watanzania hivyo chama cha ADC kimekuja kuwakomboa watanzania na kuleta upinzani wa kweli katika siasa za tanzania .
HAMAD RASHID ni mgombea wa Urais wa Chama hicho kwa upande wa Zanzibar ambapo leo pia alikuwa mmoja kati ya viongozi waliomsindikiza mgombea huyo katika nkuchukua Form ya kuwania Urais.
 Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad