![]() |
Mbunge wa
Baruadi Mgharibi, Andrew Chenge (kushoto) akipangua hoja za mwanasheria wa
serikali aliyembele ya mwenyekiti wa Tume ya Maadili. |
![]() |
Mwenyekiti wa tume ya maadili ya viongozi wa umma, Jaji mstaafu , Hamis Msumi(katikati) pembeni yake ni viongozi wengine wa baraza hilo. |
![]() |
Chenge
akijiandaa kuondoka mara baada ya kuahirishwa kikao.
|
![]() |
..akisalimiana
na mmoja wa viongozi wa baraza la maadili baada ya kuahirishwa.
|
![]() |
Chenge
akitoka lango kuu la Ukumbi wa Karimjee.
TUME ya
Maadili chini ya Baraza la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, leo August
07,2015 katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar imezidi kumhoji, Mwanasheria Mkuu
wa zamani, Andrew Change ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi anayemaliza
muda wake anayetuhumiwa kupata mgawo wa fedha za Tegeta Escrow anazodaiwa
kupata kutoka kwa mmiliki wa Kampuni ya VIP Engineerung, James Rugemalira.
Awali
Mwanasheria huyo alifikishwa mbele ya baraza hilo akidaiwa kukiuka sheria ya
maadili ya viongozi wa umma kwa kupata mgawo wa fedha kutoka kwenye akaunti
hiyo ambazo zinakadiriwa kuwa ni sh. bilioni 1.6.
Akizungumza
mbele ya Mwenyekiti wa Baraza la Maadili, Jaji Hamis Msumi, Chenge alikanusha
kuwa hahusiki na tuhuma za fedha za Escrow na wala hajawahi kuwa na mgongano wa
maslahi kati ya IPTL na VIP.
Chenge
alisema kuwa aliingia mkataba na Kampuni ya VIP katika kutoa ushauri wa
kisheria dhidi ya kampuni binafsi zilizowekeza IPL na kwamba hakuiingia mkataba
wa makubaliano na kampuni hiyo ambayo iliingia mkataba na serikali.
Mambo
yaliyoainishwa na shahidi wa upande wa serikali ni pamoja na kutumia wadhifa
wake kama mtumishi wa umma kupata maslahi binafsi ambayo ni kinyume cha kifungu
cha sheria, huku akidai kuwa Chenge amejihusisha na mngongano wa maslahi
kutokana na uchunguzi uliofanyika katika vipindi mbalimbali akiwa mwanasheria
mkuu wa serikali.
Change
akipangua hoja za mwanasheria wa serikali alisema kuwa serikali iliingia mktaba
wa makubaliano ya kuzalisha umeme na Kampuni ya IPL wakati akiwa mwanasheria na
baada ya kustaafu aliingia makubaliano ya mdomo na mmiliki wa VIP ya kutoa
ushauri kuhusu masuala ya kitaalamu kwa IPL tu.
Mwenyekiti
wa baraza hilo Jaji Mstaafu, Hamis Msumi aliahirisha kusikilizwa kwa shauri
hilo kwa madai ya kuwa upande wa wanasheria wa serikali uende kuandaa taarifa
iliyosahihi ili kumpelekea Chenge Agosti 11 kwa ajili ya kupitia na baadaye
taarifa hizo kupelekwa kwa mwenyekiti wa tume Agosti 14 kwa ajili ya kutoa
uamuzi sahihi.
(NA DENIS
MTIMA/GPL)
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment