Alivyoachishwa
kazi
Kama
ilivyowahi kuelezwa na gazeti hili, wakazi wa Chato wanaamini kuwa Dk Magufuli
hakuwa na ndoto za kuwa mwanasiasa mpaka aliposhawishiwa na wazee kugombea
ubunge baada ya kuona wamekuwa wanyonge kwa muda mrefu.
Mzee Emmanuel
Francis anayakumbuka maisha ya ujana ya Magufuli, ‘’Wazee tulikaa na kumuona
huyu ndiye msomi wa kiwango cha juu anayeweza kutukomboa tulikuwa tunamfuatilia
tangu akiwa mwalimu shule ya sekondari Sengerema hata alipokuwa mkemia kwenye
shirika la pamba,” alibainisha Francis.
Anasema
Magufuli hakuwakatisha tama, alikubali kujitosa kugombea ubunge akipambana na
Phares Kabuye (sasa marehemu) ingawa matokeo hayakukidhi kiu yao, japokuwa
mgombea mwenyewe aliyakubali.
Tukio la
Magufuli kumshika na kumpongeza mshindani wake liliwashangaza na kumuona kama
kijana asiye na kinyongo.
KIlichomponza
hata hakina maana, wanasema hata uvaaji wake wa miwani ulimpunguzia kiasi
fulani cha kura baada ya baadhi yao kuamini kuwa miwani ni kielelezo cha usomi
na hivyo asingekuwa kiongozi wa kukimbiliwa.
‘’Wasukuma
tuna kasumba ya kupigiwa magoti, baadhi ya wananchi walipomuona ni kijana
anayependa kuvaa miwani walisema huyu ndiye atatusahau kabisa,” anabainisha
Francis.
Alipojaribu
mara ya pili baada ya jimbo kutengwa na kuanzishwa Chato akaibuka mshindi, sasa
wanajivunia kuwa na shule nyingi za sekondari zikiwamo wa Muungano, Meghji na
Chato na nyingine zikiwa na kidato cha tano na sita, suala ambalo Francis
anasema lisingewezekana bila Dk Magufuli.
Tetesi za
urais
Wanakijiji
wenzake wanakiri kuvuma kwa jina la mbunge wao na kutajwa miongoni mwa
waliokuwa wanataka kuwania urais katika.
Francis
anasema hana wasiwasi na kutajwa kwa jina la mbunge wake miongoni mwa wanataka
uongozi wa nchi kwa kuwa amepata uzoefu mkubwa kupitia wizara alizoongoza
katika awamu tofauti.
“Amepita
katika wizara nyingi bila kuwa na tuhuma za ubadhilifu kama ilivyotokea kwa
mawaziri wengine, alionyesha uadilifu na kila wizara aliyoongoza ilionekana
kuwa imara na yenye mafanikio,” alisema Francis.
Tangu awali,
mzee huyo na wenzake walibainisha kuwa wanatamani mbunge huyo achukue fomu ya
kugombea nafasi ya urais, huku akiamini kuwa anaweza kuungwa mkono na wananchi
wengi kutokana na historia yake ya kuwatumikia kwa uadilifu.
Hata hivyo,
wasiwasi wa wengi ni kuwa waadilifu wa aina yake ni vigumu kupata nafasi hadi
kufikia kiwango cha kupendekezwa kuwania uongozi wa nchi kwa kuwa kuna makundi
hayawapendi.
Mchunga
ng’ombe
Familia ya
Magufuli ambaye ni baba yake na John ilikuwa ya wafugaji, hivyo watoto
waliozaliwa katika kaya hiyo kwa vyovyote vile wasingeweza kulikwepa jukumu la
kuchunga ng’ombe.
Hata wakati
wa likizo wananchi walizoea kumuona John akifanya kazi za kawaida za nyumbani
ikiwa ni pamoja na kuchunga ng’ombe na kukamua maziwa wakati wa likizo.
“Baba yake
alikuwa na mifugo mingi na hakuwa mtu wa kujikweza, wakati wa likizo tulizoea
kumuona John akifanya kazi za nyumbani hata kwenda shambani kulima na kukamua
maziwa,” alisema mkazi wa kijiji hicho.
Mkazi
mwingine, Maritha Rufunga ana kumbukumbu tofauti kuhusu maisha ya ujana wa
mbunge huyo na hata hajasahau wakati mbunge huyo kwa sasa alipoanza safari yake
kielimu kwa kujikwaa.
“Hakuwa na
majivuno na hata alipomaliza shule na kushindwa kuchaguliwa baba yake alikuwa
amekataa asiendelee na masomo, lakini kuna mwalimu wake alikwenda kumtetea kwa
baba yake ili akarudie shule,” alisema Maritha Rufunga.
Source:-Mwananchi
Jumamosi.
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment