Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva
(wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza majimbo
mapya ya uchaguzi katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam leo
Julai 13,2015.
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza majimbo 26 mapya ya uchaguzi
ambayo yatakuwa na wagombea katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka
huu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kukata kwa majimbo hayo
wamezingatia idadi ya watu pamoja na Jiografia
katika majimbo mapya.
Amesema katika upande wa Zanzibar majimbo yamebaki kuwa 50 kama awali
hiyo inatokana vigezo vilivyowekwa na tume hiyo.
MAJIMBO YALIYOANZISHWA KWA KIGEZO CHA ONGEZEKO LA
HALMASHAURI
Majimbo 20 yanayoanzishwa kutokana na kuanzishwa kwa
Halmashauri mpya ni:-
1. Handeni Mjini
2. Nanyamba
3. Makambako
4. Butiama
5. Tarime Mjini
6. Tunduma
7. Nsimbo
8. Kavuu
9. Geita Mjini
10. Mafinga Mjini
11. Kahama Mjini
12. Ushetu
13. Nzega Mjini
14. Kondoa Mjini
15. Newala Mjini
16. Mbulu Mjini
17. Bunda Mjini
18. Ndanda
19. Madaba
20 Mbinga Mjini
MAJIMBO YALIYOANZISHWA KWA KIGEZO CHA IDADI YA WATU.
Majimbo 6 yanayoanzishwa kutokana na idadi ya watu ni:-
1. Mbagala – Dar es salaam
2. Kibamba – Dar es salaam
3. Vwawa – Mbeya
4. Manonga - Tabora
5. Mlimba - Morogoro
6. Ulyankulu - Tabora
Jaji Lubuva amesema baadhi ya wabunge wamekuwa wakiingia katika
Halmashauri mbili hivyo kuweka mipaka katika maeneo ili mbunge aweze kushiriki
katika Halmashauri moja tu.
Amesema baadhi majimbo yamebadilishwa majina na kuendelea kuwepo kwa
majimbo hayo kisheria.
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment