KITUO CHA POLISI STAKISHARI-UKONGA CHAVAMIWA:-IGP Ernest Mangu amefika eneo la tukio na ametangaza msako wa nguvu kuwasaka waliohusika. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, July 13, 2015

KITUO CHA POLISI STAKISHARI-UKONGA CHAVAMIWA:-IGP Ernest Mangu amefika eneo la tukio na ametangaza msako wa nguvu kuwasaka waliohusika.

Askari Polisi kadhaa, mgambo na raia  wameuwawa kikatili na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi waliovamia  kituo  cha Polisi cha Sitakishari, Ukonga,  jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo Julai 13,2015.. Silaha kadhaa pia inasemekana zimeporwa na majambazi hayo.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu amefika eneo la tukio na ametangaza msako wa nguvu kuwasaka waliohusika na tukio hilo na kukomboa silaha zilizoporwa.

Kwa mujibu wa taarifa za awali ambazo bado hazijathibitishwa na Jeshi la Polisi ni kwamba watu hao walifika kituoni hapo wakiwa katika pikipiki wakidai kwamba walikuwa wamembeba mtu aliyepata ajali wakihitaji msaada wa polisi kabla ya kuwabadilikia ghafla na kuanza kuwashambulia kwa risasi.

Inadaiwa kuwa askari wanne wamepoteza maisha katika tukio hilo, wananchi wawili na mmoja wa magaidi hao.

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad