CHAN 2016 RWANDA:-Taifa Stars yatupwa nje kwa jumla ya magoli 4-1 na Uganda. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, July 05, 2015

CHAN 2016 RWANDA:-Taifa Stars yatupwa nje kwa jumla ya magoli 4-1 na Uganda.


Mshambuliaji wa Taifa Stars, John Bocco akishangilia goli lake kwa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premieum Lager kikiwa  chini ya kocha mzawa Charles Boniface Mkwasa kimelazimisha sare ya kufungana goli 1-1 na timu ya Taifa ya Uganda ‘The Cranes’ kwenye mchezo uliomalizika jana Julai 04,2015 kwenye uwanja wa Nakivubo Kampala, Uganda ukiwa ni mchezo wa kuwania kufuzu kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN) mwakani 2016 nchini Rwanda.



Mshambuliaji wa Taifa Stars, Rashid Mandawa (kushoto) akijaribu kumtoka Hassan Waswa.

Goli la Stars liliwekwa kambani na John Bocco ‘Adebayor’ kwa mkwaju wa penati baada ya mlinzi wa Uganda kuunawa mpira akiwa kwenye eneo la hatari na mwamuzi wa mchezo kuamuru ipigwe penati, ndipo Adebayor alipoiandikia Stars goli hilo.

Lakini Uganda walisawazisha goli hilo dakika chache baadae kupitia kwa Robert Sentongo baada ya mabeki wa Stars kutegeana kuondosha mpira kwenye eneo lao la hatari na kufanya matokeo kuwa 1-1.

Matokeo hayo  yanaifanya Taifa Stars kutupwa nje kwa jumla ya magoli 4-1 baada ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa goli 3-0 na jana Julai 04,2015 kutoka sare ya kufungana goli 1-1 na kuwaacha Uganda wakisonga mbele kwenye michuano hiyo ya CHAN.

Kikosi cha Stars kilichoanza dhidi ya Uganda.

Mara baada ya mchezo huo kocha mkuu wa Taifa Stars, Charles Mkwasa amesema anashukuru vijana wake wamejitahidi kucheza vizuri, mchezo ulikua mzuri, timu ilitengeneza nafasi chache na kuweza kutumia nafasi moja iliyopatikana.

Mkwasa amewaomba watanzania kuendelea kuwapa sapoti kwani wamekaa na kwa wiki moja tu lakini imeonesha mabadiliko , hivyo wanahitaji muda mrefu kukaa na vijana ili kujenga timu bora.

Stars inatarajiwa kurejea Tanzania siku ya Jumatatu mchana kwa usafiri wa shirika la ndege la Rwanda Air.

Baadhi ya Watanzania waliokwenda Uganda kuipa sapoti  Timu ya Taifa ya Tanzania –Taifa Stars.

Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika Uganda 1 - 1 Tanzania. Kwa matokeo hayo Uganda wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla ya mabao 4 - 1 na sasa watakutana na Sudan.

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad