Rais wa
Baraza la Vyama vya Soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, Leodgar Tenga
leo ametangaza kuanza kwa michuano ya kombe la Kagame itakayoanza kutimua vumbi
Julai 18, 2015 na kumalizika Agosti 2 mwaka huu jijii Dar es salaam.
Akiongea
na waandishi wa habari leo ,Julai 01,2015 katika ofisi za TFF zilizopo Karume, Tenga
ameishukuru serikali ya Tanzania na TFF kwa kukubali kuwa wenyeji wa michuano
hiyo mikubwa, vyombo vya habari na wapenzi wa mpira wa miguu nchini kwa sapoti
yao na kuipokea kwa mikono miwili michuano hiyo.
Lengo la
CECAFA ni kuona vilabu vya ukanda huu vinapata nafasi ya kucheza michezo mingi
na kujiandaa kwa ajili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho
barani Afrika.
Naye Rais
wa TFF, Jamal Malinzi amewashukuru CECFA kwa kuipa Tanzania uenyeji huo na
kuahidi TFF itahakikisha michuano hiyo inafanya nchini katika hali ya amani na
usalama toka mwanzo mpaka mwisho wa michuano hiyo.
Timu zilizothibtisha
kushiriki michuano hiyo ni:-
Yanga SC na Azam FC (Tanzania).
APR (Rwanda).
Gor Mahia
(Kenya)
Telecom (Djibout)
KMKM (Zanzibar)
Khartoum-N (Sudan)
Al Shandy
(Sudan)
LLB AFC (Burundi)
Heegan FC (Somalia)
Malakia (Sudani Kusini)
Adama
City (Ethiopia)
na
KCCA (Uganda).
Wakati huo
Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholaus Musonye ametangza ratiba ya michuano ya Kombe
la Kagame itakayoanza kutimua vumbi Julai 18, 2015 jijini Dar es salaam
ikishirikisha timu 13 kutoka nchi wanachama wa CECAFA.
Mechi ya
ufunguzi tarehe 18 Julai, 2015 Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam itashuhudia
wenyeji Yanga SC wakicheza na Gor Mahia ya Kenya, huku APR ya Rwanda ikicheza
na Al Shandy ya Sudan na KMKM ya Zanzibar wakifungua dimba na Telecom ya
Somalia.
Ratiba ya
michuano hiyo imeziweka timu hizo katika makundi matatu ambapo kundi A lina
timu za:-
Yanga (Tanzania),
Gor Mahia (Kenya),
Telecom (Djbiout),
KMKM
(Zanzibar)
na
Khartoum-N (Sudan)
Kundi B:-
APR (Rwanda),
Al Shandy (Sudan),
LLB AFC (Burundi)
na
Heegan FC (Somalia)
Kundi C:-
Azam FC (Tanzania),
Malakia (Sudan Kusini),
Adama City (Ethiopia)
na
KCCA (Uganda)
Timu tatu
zitakazoshika nafasi ya juu kutoka kundi A, timu mbili za juu kutoka kundi B
& C, na mshindi mwenye wastani mzuri kutoka kundi B & C zitaingia katika
hatua ya robo fainali.
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
Wednesday, July 01, 2015
CECAFA:- Hii ndiyo Ratiba ya Kagame CUP 2015 iliyotolewa leo Julai 01,2015 .
Tags
# MICHEZO
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
MICHEZO
Labels:
MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment