Rais wa
Burundi,Bw. Pierre Nkurunziza akiwasili kwenye kituo cha kupiga kura kwa
usafiri wa baiskeli hapo jana June 29, 2015. |
Rais Nkurunziza akiwa kwenye foleni kwenda kupiga kura yake ya kumchagua mbunge. |
Rais
Nkurunziza akipiga kura yake.
RAIS wa
Burundi, Pierre Nkurunziza Jana June 29, 2015 amepiga kura katika eneo la Ngozi kwa ajili ya
kumchagua mbunge wa Jimbo lake.
Nkurunziza
amewasili katika kituo cha kupigia kura akitumia usafiri wa baiskeli akiwa
amesindikizwa na wapambe wake.
Baadaye rais
huyo anayetaka kuwania URAIS kwa muhula
wa tatu alijipanga kwenye foleni ili apige kura huku pembeni yake wakiwepo
walinzi wake.
Aidha uchaguzi
wa wabunge unaendelea nchini Burundi
licha ya maandamano na ghasia dhidi ya uamuzi wa Rais Pierre Nkurunziza wa
kutaka kuwania muhula wa tatu.
Upinzani umesusia uchaguzi huo huku
Muungano wa Ulaya ukieleza kuwa uchaguzi huo utazidisha mgogoro uliopo.
Umoja wa
Afrika (AU) umekataa kutoa waangalizi ukisema kuwa baadhi ya masharti
yaliowekwa hayajaafikiwa kwa uchaguzi kuwa huru na haki.
Zaidi ya
watu 70 wameuawa tangu mgogoro huo uanze huku takribani watu 130,000
wakilitoroka taifa hilo.
Picha na BBC
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment