Mtoto
Emmanuel Sandu aliyefariki miaka 12 iliyopita katika Kijiji cha Idahina
wilayani Kahama Mkoani Shinyanga ameonekana akiwa hai jambo lililoibua hofu
miongoni mwa Wakazi wa Kijiji hicho.
Wazazi wa
Mtoto huyo mwenye miaka 15 kwa sasa, wamesema mtoto wao alifariki mwaka 2002
akiwa na umri wa miaka Miwili na kwamba wamemtambua kutokana na Alama
waliyomuwekea usoni wakati akisumbuliwa na tatizo la Michango.
Wazazi hao
Bw Sandu Usila na Shalu Lusegembe wamesema tukio la kupatikana kwa mtoto wao
linahusishwa na Imani za Kishirikina na kwamba mtoto huyo alichukuliwa kwa
nguvu za giza na kuwekwa Msukule.
Mtendaji wa
Kata hiyo Bw Isack Madela amesema ofisi yake inawasiliana na Jeshi la Polisi
wilayani Kahama kwa ahtua zaidi na kwamba kutokana na msongamano mkubwa wa watu
waliojaa ofisini kwake kumshuhudia mtoto huyo, ameamua kumkabidhi kwa wazazi wake.
Bw Madela
amesema mtoto huyo hawezi kuzungumza huku mwili wake ukiwa umedhoofika na
kwamba anapoulizwa jina anataja moja pekee la Emmanuel hali inayoonesha kuwa
alikuwa akiishi kwenye mazingira yasiyo ya Kibinadamu.
Habari kwa hisani ya RADIO KWIZERA FM.
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
Thursday, June 25, 2015
TAHARUKI YA USHIRIKINA:-Mtoto aliyefariki miaka 12 iliyopita ameonekana akiwa hai .
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment