Picha kwa
hisani ya Father Kidevu.
Mkwasa
amesema cha kwanza atakachokifanya na msaidizi wake Morocco ni kurudisha imani
ya watanzania juu ya timu yao ya Taifa, kisha watajitahidi kadri ya uwezo wao
kuhakikisha kuwa timu inafanya vizuri katika michezo inayowakabili.
Ametangaza
kikosi cha wachezaji 26 watakaoingia kambini kesho alhamisi katika hoteli ya
Tansoma tayari kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda.
Akizungumza
na waandishi wa habari hii jana June 25,2015, alisema ‘Baada ya kutangaza kikosi cha
wachezaji ambacho kitakuwa na kazi ya kubadili matokeo ya kufungwa mabao matatu
kwa sifuri na kusaka ushindi wa zaidi ya mabao manne kwa sifuri ugenini huko
jijini Kampala mnamo July 04,2015′
WALIOACHWA:
Kipa Deogratius
Munish ‘Dida’ na nafasi yake amemchagua Ally Mustapha ‘Barthez’ , wengine ambao
Mkwasa amewatema ni Erasto Nyoni, Amri Kiemba na Kelvin Friday kutoka Azam FC
pia Oscar Joshua kutoka Yanga, Pia Ibrahim Ajibu kutoka Simba .
Waliorejea ni Kelvin Yondani pia Deus Kaseke huku
akimchukua Michael Idan wa Ruvu Shooting.
Pia Samuel
Kamuntu wa JKT, Juma Abdul wa Yanga na Mudathir Yahya kutoka Azam wamejumuishwa
kwamba wanaweza kuitwa wakati wowote.
KIKOSI KAMILI:
Mwadini
Ally-Azam
Ally
Mustapha-Yanga
Mudathir
Khamis-KMKM
Shomari
Kapombe-Azam
Michael
Haidan-Ruvu Shooting
Mohammed
Hussein-Simba
Mwinyi
Hajj-KMKM
Nadir
Haroub-Yanga
Kelvin
Yondani-Yanga
Aggrey
Morris-Azam
Hassan
Isihaka-Simba
Jonas
Mkude-Simba
Abdi Banda-Simba
Simon
Msuva-Yanga
Said
Ndemla-Simba
Ramadhan
Singano-Simba
Salum
Telela-Yanga
Frank
Domayo-Azam
Atupele
Green-Kagera Sugar
Rashid
Mandawa-Mwadui
Ame
Ally-Azam
Deus
Kaseke-Yanga
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment