EPL 2014/2015:-Huu ndio Msimamo wa Ligi baada ya Chelsea,Arsenal na Manchester United kushinda mechi zao Jana April 04, 2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, April 05, 2015

EPL 2014/2015:-Huu ndio Msimamo wa Ligi baada ya Chelsea,Arsenal na Manchester United kushinda mechi zao Jana April 04, 2015.

Vinara wa Ligi Kuu Uingereza msimu huu wa 2014/2015, Chelsea wameendelea kujiimarisha kileleni mwa Ligi baada ya kuifunga Stoke City Bao 2-1 Uwanjani Stamford Bridge ,hapo jana April  04, 2015.


Ushindi huu umeipa Chelsea Pointi 70 kwa Mechi 30 wakifuatiwa na Arsenal wenye Pointi 63 kwa Mechi 31 kisha Man United wenye Pointi 62 kwa Mechi 31 na Man City wako Nafasi ya 4 wakiwa na Pointi 61 kwa Mechi 30.

Mabao ya Mechi jana yalifungwa na Eden Hazard kwa Penati ya Dakika ya 39 baada Cesc Fabregas kuchezewa faulo lakini Stoke walisawazisha Dakika ya 44 kwa Bao zuri sana la Charlie Adam alipomfuma Kipa wa Chelsea Courtois akiwa ametoka Golini na yeye kurusha kombora la juu kutoka Mita 65, upande wa Uwanja wa Stoke, na kutinga wavuni.

Mechi nyingine ilikuwa huko uwanja wa  Emirates Jijini Londo, Arsenal nao wakaichapa Liverpool Bao 4-1 na kuchupa hadi Nafasi ya Pili ya msimamo wa Ligi Kuu ,kwa  Magoli ya Hector Bellerin, Mesut Ozil na Alexis Sanchez.

Kipindi cha Pili Liverpool walipata Bao lao pekee kwa Penati ya Nahodha wao Jordan Henderson iliyotolewa baada ya Raheem Sterling kuchezewa faulo.

Arsenal walipiga Bao la 4 kupitia Olivier Giroud na Gemu kwisha kwa ushindi wao wa 4-1.  


Nao Manchester United wakiwa nyumbani kwao Old Trafford wakaichapa Aston Villa 3-1 , kwa Bao la Ander Herrera la Dakika ya 43 na Kipindi cha Pili kupiga Bao 2 nyingine katika Dakika ya 79 kupitia Nahodha Wayne Rooney na Ander Herrera Dakika ya 90.

Bao pekee la Villa lilifungwa na Christian Benteke katika Dakika ya 80.

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila tukio/stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad