Hatimaye mchezaji Fabrice Muamba atangaza kuachana na soka rasmi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, August 15, 2012

Hatimaye mchezaji Fabrice Muamba atangaza kuachana na soka rasmi.


Mchezaji wa kiungo cha kati wa Bolton na timu ya taifa ya Uingereza , Fabrice Muamba ametangaza kuwa amestaafu kama mchezaji wa kulipwa wa soka.


Muamba, mwenye umri wa miaka 24 na mwenye asili ya Congo alizirai na kupata mshutuko wa moyo tarehe kumi na saba mwezi Machi mwaka huu wakati Bolton ilipokuwa ikichuana na Tottenham Hotspurs.


Akiongea na waandishi wa habari Muamba, alisema licha ya habari hizo kuwa za kuhuzunisha, anawashukuru mashabiki wake na wasimamizi wa klabu hiyo.



''namshukuru mungu kuwa niko hai hii leo na kwa mara nyingine nawashukuru sana madaktari wote ambao hawakufa moyo wakati nilikuwa na matatizo'' alisema Muamba.


Muamba pia ameshukuru kwa maombi na sapoti kubwa aliyoipata kutoka kwa wapenzi wote wa soka duniani.


Aidha Moyo wa Muamba ulisimama kwa saa 78 baada ya kudondoka kwenye dimba la White Hart Lane baada ya kupatwa mshtuko wa moyo hali iliyopelekea kufanyiwa matibabu na kuweza kuokoa maisha yake.




Alikaa mwezi mzima Hosptali lakini aliwashangaza madaktari kwa jinsi alivyopata nafuu kwa haraka huku akisistiza anataka urudi kwenye dimba aendelee kucheza soka.



Kiungo huyo wa Bolton na Uingereza alienda mpaka nchini Ubelgiji wiki iliyopita kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji mdogo ili kuweza kuwa fiti kwa ajili kurudi uwanjani.

 

Kabla ya kutangaza kustaafu Mumba aliwaambia mashabiki wake waendelee kutabasamu na kila kitu kitakuwa poa.


Historia yake ya soka na kuanza kujulikana ilianzia katika academy ya soka ya Arsenal mwaka 2002 kabla ya kuhamia Birmingham na baadae akaenda Bolton mwaka 2008.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad