Diamond Platnumz’ akiwa na Idris na Samantha BBA.
MFALME
DIAMOND
Baada ya Mzee Yusuf ambaye alidhihirisha kuwa ni mkali na kuweka rekodi yake,
shangwe kubwa liliibuka pale Diamond alipopanda stejini, ilikuwa saa 7:38 usiku
na kuanza kufanya yake kama ilivyo kawaida mashabiki walimpokea kwa kumuita
afande.
Diamond
alianza kutoa shoo kwa kupiga baadhi ya nyimbo zake, Kamwambie, Nitarejea,
Mdogomdogo, Ntampata Wapi na nyingine nyingi kama ‘play back’ na kuhamia kwenye
‘live band’ ambapo aliimba nyimbo za Mawazo, Moyo Wangu na Nimpende Nani na
kufuatiwa na sebene la nguvu.
Diamond
hakuishia hapo, alikuja na ‘sapraiz’ kwa mashabiki kwa kumpandisha jukwaani
Mshindi wa Shindano la Big Brother Africa ‘Hotshots’ 2014, Idris Sultan ambaye
alitoa shukrani kwa mashabiki:
“Kile nilichokuwa nikiahidi kwa mashabiki ambao walikuwa wakinipigia kura sasa
ndiyo naanza kutekeleza kama ifuatavyo, na leo nimekuja hapa kwenu kutoa
shukrani zangu za dhati.“Ninaomba nimtambulishe mshiriki mwenzangu kutoka
Afrika Kusini, Samantha (shori mkali) ambaye ndiye rafiki yangu.
|
No comments:
Post a Comment