Aliongeza
kuwa, kwa hali ilivyo wananchi wanahitaji mabadiliko na kwamba mchakato wa
katiba ulikuwa njia mzuri ya kuanzisha mabadiliko hayo, lakini akadai mchakato
mzima umevurugwa na hakuna dhamira ya mabadiliko ya kweli.
Kuhusu suala
la daftari la kupiga kura, Mbowe alisema daftari hilo linapaswa kuboreshwa kwa
kuwa kuna idadi kubwa ya wananchi hawakuandikishwa, hivyo kwenye uchaguzi mkuu
ujao watakosa haki yao ya kupiga kura.
Pamoja na
mambo mengine, kikao hicho pia kilijadili agenda mbalimbali 11 na kufanya
uteuzi wa bodi ya wadhamini wa chama hicho, kufanya uteuzi wa makatibu wa
wilaya na mikoa na kujadili mapendekezo ya katiba pamoja na kupokea taarifa ya
ukaguzi wa hesabu za chama hicho.
|
No comments:
Post a Comment