Nchi ya Tanzania hii leo October 14,2014, inaadhimisha kumbukumbu ya
miaka kumi na mitano tangu kifo cha baba wa taifa letu,Mwalimu Julius Kambarege
Nyerere ambaye aliaga dunia tarehe 14 mwezi 10 mwaka 1999.
Hii leo
nchini Tanzania ni siku ya mapumziko, wakati huu ambapo wananchi wametakiwa
kuendelea kuyaenzi yale mazuri aliyowaachia hayati Baba wa Taifa ambaye wakati
wa uhai wake alisisitiza suala la amani na Umoja miongozi mwa watanzania na
bara la Afrika.
Watanzania
wengi wanamkumbuka Baba wa Taifa ,Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye
alifariki Octoba 14 mwaka 1999 ikiwa ni miaka 15.
Watanzania
wanamuenzi mwalimu kwa mengi lakini kuu ni ile falsafa yake ya umoja ambayo
ilimpelekea kuunganisha Tanganyika na Zanzibar.
Mwalimu
Nyerere anaheshimiwa na watanzania wengi kwa uadilifu na moyo wake wa kutumikia
kuliko kutumikiwa.
|
No comments:
Post a Comment