Pichani juu na chini ni Waokoaji wakiwa wamebeba mwili uliopatikana kutoka
ziwa Tanganyika baada ya ajali ya Mitumbwi katika kijiji cha kalalangabo.
Kaimu Kamanda
wa Polisi mkoani Kigoma, Bw Dismas Kisusi amewataja waliopatikana leo asubuhi
wakiwa tayari wamefariki kuwa ni Masoud Ally, Rehema Kassim, Fitina Issa, Hawa
Lwampata, Jackob Rashidi, Mohamud Ulimwengu na Hawa Gamba
Kamanda
Kisusi amesema zoezi la uokoaji linafanywa kwa ushirikiano wa Jeshi la Polisi,
Jeshi la Ulinzi la Wananchi JWTZ pamoja na wavuvi na kwamba haijafahamika idadi
ya watu ambao bado hawajapatikana
Mitumbwi
hiyo imepata ajali juzi Jumamosi na kwamba kwa kawaida hupakia watu 20 lakini
inadaiwa kuwa ilikuwa na watu zaidi ya 70 hali iliyosababisha kuzama baada ya
kukutana na dhoruba muda mfupi baada ya kuanza safari kuelekea kijiji cha
Kigalye mwambao wa ziwa Tanganyika
|
No comments:
Post a Comment