Kijana Paulo Simon(majeruhi) akiandika maelezo
kwa Polisi kwa njia ya maandishi.
“Sikuwa na
mazoea naye, nilipokataa kufanya naye mapenzi, alinisogelea na kunishika sehemu
zangu za siri na kuanza kuzivuta, nilipopiga kelele akanishika kichwa na
kunilazimisha ‘kunidendesha’, akafanikiwa kuingiza mdomo wake kwangu na
kunikata ulimi wangu, akaondoka nao na kwenda kuutema karibu na mlango wa bar,”
alisema Simon ambaye wahudumu wa hospitali hiyo wamelazimika kumwekea ndoo ili
awe anatemea damu kutokana na kujaa mdomoni.
Alisema
baada ya kukatwa ulimi ambao sasa unamletea maumivu makali, alifanikiwa kufika
nyumbani kwake kabla ya tajiri yake kumchukua na kumpeleka hospitalini ambako
amelazwa.
Jeshi la Polisi mkoani Arusha limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba
mtuhumiwa ameshatiwa mbaroni huku uchunguzi ukiwa unaendelea. Hali ya majeruhi
inaendelea vizuri.
Habari Na:-
Joseph Ngilisho- Arusha/GBL
|
No comments:
Post a Comment