Meneja huyo,
Julius Gashaza, ambaye alikuwa na jukumu la kupanga bei za mafuta za kila
mwezi, alihudhuria kikao hicho mjini Dodoma kwa siku mbili; Ijumaa na Jumamosi
iliyopita kuhusu mambo mbalimbali, yakiwamo kiwango cha mafuta kinachoingizwa
nchini, mgawo wa fedha unaotolewa na Ewura kwenda kuhudumia umeme vijijini
(Rea) na fedha za mfuko wa barabara.
Jeshi la
Polisi, Mkoa wa Temeke limethibitisha tukio hilo na kueleza kuwa meneja huyo
alikutwa amejinyonga kwa kutumia tai kwenye hoteli ya Mwanga Lodge iliyopo
Yombo Vituka wilayani Temeke.
Nyumbani kwa
meneja huyo wa Ewura, kulikuwa na waombolezaji waliokuwa kwenye vikundi na
kikao cha maandalizi ya mazishi kilifanyika ndani ya nyumba ya marehemu iliyopo
Yombo Vituka na baadaye kuhamia nyumba ya jirani.
Kamati ya
Bunge ya Bajeti, inayoongozwa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge,
ilikutana na maofisa wa Ewura, akiwamo Gashaza na wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) na kugundua kuwapo kwa tofauti katika takwimu za kiwango cha mafuta
kilichostahili kutozwa kodi.
Gashaza
alikwenda Dodoma kutoa ripoti ya Ewura kwenye kamati hiyo ya Bunge
akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Felix Ngamlagosi.
Kwa mujibu
wa taarifa kutoka ndani ya kamati hiyo, takwimu za Ewura ziliashiria kuwa fedha
zilizopatikana ni nyingi zaidi ya zile zilizoelezwa na TRA, lakini Wizara ya
Fedha ilisisitiza zifuatwe takwimu za mamlaka ya mapato.
Habari hizo,
zinasema baada ya kurejea Dar es Salaam juzi majira ya saa tatu usiku, Gashaza
hakwenda nyumbani kwake na badala yake alikwenda kwenye hoteli iliyo karibu na
nyumbani ambako mkewe na ndugu yake mmoja walimfuata na akawaeleza kuwa anahisi
kutishiwa maisha yake.
Baadaye
walifanya maombi maalumu kabla ya kuachana naye.
Inadaiwa
kuwa marehemu aliomba akalale hotelini kwa sababu hakuona kama ana amani kulala
nyumbani kwake na ilipofika asubuhi alikutwa ‘amejinyonga’ ndani ya chumba
alicholala hotelini humo.
Nyumbani kwa
marehemu waombolezaji walikusanyika katika makundi, lakini baada ya kukaa
katika kikao cha familia walitoka na kauli moja kuwa hawatasema chochote na
kwamba jukumu hilo libaki mikononi kwa polisi.
Polisi
wathibitisha....''
Habari Na:-Mwananchi.
hajajinyonga kauawa
ReplyDelete