![]() |
Wachezaji wa
Arsenal wakiwa na nyuso za kusikitika baada ya Walters alikwenda kuukwamisha
nyavuni mkwaju huo dakika ya 76 baada ya Laurent Koscielny wa Arsenal kuunawa
mpira kwenye eneo la hatari.
|
![]() |
Jonathan
Walters akishangilia na Peter Crouch baada ya kufunga penalti iliyoipa Stoke
ushindi wa 1-0.
|
Jana March
01,204,Chelsea ilizidi kupaa kileleni mwa Ligi kuu soka Uingereza baada ya
kuifunga Fulham Bao 3-1 huku Bao la Fulham lilifungwa na Johnny Heitinga wakati
Arsenal, ambayo iko Nafasi ya Pili nyuma yao, kupigwa Bao 1-0 na Stoke City.
Penati ya dakika
ya 76 ya Jonathan Walters iliwapa ushindi Stoke City wa Bao 1-0 walipopambana
kwao Britannia Stadium na Arsenal ambao pigo hili limewaacha wakiwa Pointi 4
nyuma ya Vinara Chelsea.
Penati hiyo
ilitolewa baada ya Sentahafu Laurent Koscielny kuunawa Mpira.
Kipigo hiki
kimeifanya Arsenal iwe imeshinda Mechi 1 tu kati ya 8 zilizopita ndani ya
Britannia Stadium na hata ushindi huo Mwaka 2010 haukuleta raha kwani ni Siku
hiyo Aaron Ramsey alivunjwa Mguu vibaya.
Pia kipigo
hiki kimekuja wakati mbaya kwa Arsenal katika azma yao ya kutwaa Ubingwa Msimu
kwa vile Wapinzani wao wanaofuata ni Tottenham, Chelsea na Manchester City
ambao watapambana nao ndani ya Wiki mbili.
![]() |
Luis Suarez. |
Wakicheza
Uwanja wa Saint Mary, Liverpool wameichapa Southampton Bao 3-0 na kukwea hadi
Nafasi ya Pili kutoka Nafasi ya 4 kwenye Ligi Kuu Uingereza.
Bao za
Liverpool zilifungwa na Luis Suarez, Dakika ya 16, Raheem Sterling Dakika ya 58
na Penati ya Dakika za Majeruhi ya Steven Gerrard baada ya Suarez kuangushwa na
Jose Fonte.
RATIBA/MATOKEO EPL 2013/2014.
Jumamosi
Machi 1,2014.
Everton 1
West Ham 0
Fulham 1
Chelsea 3
Hull 1
Newcastle 4
Stoke 1
Arsenal 0
Southampton 0 v Liverpool 3
RATIBA EPL.
Jumapili
Machi 2,2014.
1930 Aston
Villa v Norwich
1930 Swansea
v Crystal Palace
1930
Tottenham v Cardiff
Position | Team | Played | Goal Difference | Points |
---|---|---|---|---|
1 | Chelsea | 28 | 30 | 63 |
2 | Liverpool | 28 | 38 | 59 |
3 | Arsenal | 28 | 24 | 59 |
4 | Man City | 26 | 42 | 57 |
5 | Tottenham | 27 | 3 | 50 |
6 | Everton | 27 | 11 | 48 |
7 | Man Utd | 27 | 12 | 45 |
8 | Newcastle | 28 | -2 | 43 |
9 | Southampton | 28 | 3 | 39 |
10 | West Ham | 28 | -4 | 31 |
11 | Hull | 28 | -5 | 30 |
12 | Stoke | 28 | -14 | 30 |
13 | Swansea | 27 | -4 | 28 |
14 | Aston Villa | 27 | -10 | 28 |
15 | Norwich | 27 | -19 | 28 |
16 | Crystal Palace | 26 | -18 | 26 |
17 | West Brom | 27 | -8 | 25 |
18 | Sunderland | 26 | -16 | 24 |
19 | Cardiff | 27 | -29 | 22 |
20 | Fulham | 28 | -34 | 21 |
No comments:
Post a Comment