Tazama Taswira ya Basi la Kampuni ya Taqwa likinusurika kuwaka moto katika eneo la Mkajagali wilayani Ngara mkoani Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, December 19, 2013

Tazama Taswira ya Basi la Kampuni ya Taqwa likinusurika kuwaka moto katika eneo la Mkajagali wilayani Ngara mkoani Kagera.


Basi la Taqwa lililokuwa na zaidi ya abiria 60  ambao wamenusurika kupoteza maisha yao baada ya basi hilo walilokuwa wakisafiria kutoka Dar es salaam kupitia mjini Ngara kueleke Jijini Bujumbura nchini Burundi kunusurika kuwaka moto wilayani Ngara Mkoani Kagera.



Basi la abiria la Kampuni ya Taqwa lenye namba za usajili T 964 BHS aina ya SCANIA likiwa limenusurika kuteketea kwa moto leo( Desemba 18,2013) majira ya saa tano asubuhi katika eneo la Mkajagali kijiji cha Kumuyange, nje kidogo ya mji wa Ngara.


Kwa mujibu wa Mashuhuda ambao walikutwa na Camera ya Mwana wa makonda Blog katika  eneo la tukio,wamesema kuwa chanzo  moto huo  ni hitilafu katika mfumo wa breki wa matairi ya nyuma, yaliyotoa moshi mkubwa na kuzalisha cheche zilizosababisha moto huo kutokea na kwamba  moto huo ulifanikiwa kuzimwa kwa ushirikiano na Wananchi wa Mkajagali  na hakuna abiria aliyepata Majeraha.






Jeshi la polisi wilayani Ngara liliimarisha Ulinzi katika eneo la tukio ambapo  lilifanikiwa kumtia mbaroni kijana mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja aliyekuwa ameiba mafurushi ya bidhaa za Wasafiri huku wengine pia wakifanikiwa kupora mali za abiria na kuzificha vichakani.





Baadhi ya Wananchi waliofika kutoa msaada /kuwapokea ndugu zao wamewataka Wananchi wenzao  kuwa na moyo wa Upendo/Huruma kusaida pale ajali zinapojitokeza katika maeneo yao na kuacha tabia ya wizi wa mali pamoja na Madereva kuwa makini hasa wa mabasi yanayofanya safari kupitia  barabara ya Isaka-Ngara-Burundi yenye miteremko mikali kupunguza mwendo kasi wakati wa kutelemka miteremko hiyo ili kuepusha ajali.


Basi hilo la Taqwa lenye namba za usajili T 964 BHS aina ya SCANIA baadae lilifanikiwa kuondoka eneo la tukio kuelekea mjini Ngara kwa ajili ya Matengenezo zaidi ili liweze kuendelea na safari zake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad