Pia Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe (MB) ametoa taarifa kwa Katibu
Mkuu wa Chama kumueleza nia yake kukata rufaa Baraza Kuu la Chama kupinga
hatua iliyochukuliwa na Kamati Kuu dhidi yake kumvua nyadhifa zake ndani
ya Chama.
Kuna sababu mbili za msingi za kukata rufaa:-
1. Utaratibu wa kuchukua hatua za nidhamu ulikiukwa.
2. Sababu za kuchukuliwa hatua hizo sio sahihi.
Utaratibu ambao unatakiwa kufuatwa kabla ya kumchukulia hatua za
kinidhamu kiongozi kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Uendeshaji ni kama
ifuatavyo;
Kanuni ya Uendeshaji 6.5.6 inasema;
Taarifa kwa Vyombo vya habari 11/12/2013 Albert Msando 2
Kiongozi yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu bila kwanza kupewa
mashitaka yake kwa maandishi na mamlaka husika na kupewa nafasi ya kujibu
mashitaka kwa maandishi.
Pia tunapenda ijulikane kwamba Kanuni ya Uendeshaji 6.5.2 (a), (b),
(c) na (d) kama ilivyorekebiswa Januari 2013 inasema;
Kwa mujibu wa ibara ya 5.4.3 na 5.4.4 ya Katiba mwanachama yeyote hatachukuliwa
hatua za kinidhamu ama kuonywa ama kuachishwa ama kufukuzwa uanachama
bila kwanza;
a) Kujulishwa makosa yake kwa maandishi na kutakiwa kutoa majibu katika
muda usiopungua wiki mbili.
b) Kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika.
c) Mwanachama atajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao mnamo wiki
mbili baada ya kusikilizwa.
d) Kamati Kuu inaweza kuchukua hatua za dharura bila kuzingatia utaratibu
(b), (c) hapo juu kama itaona maslahi ya Chama kwa ujumla yanaweza kuathiriwa
isipokuwa mwanachama au kiongozi anayelalamikiwa atalazimika kuitwa kwenye
kikao husika.
Taarifa kwa Vyombo vya habari 11/12/2013 Albert Msando 3.
Naomba nichkue fursa hii kufafanua kuwa uongozi wa chama ulifanya
mkutano na waandishi mnamo tarehe 26/11/2013 na kusema kwamba marekebisho haya
ya Kanuni ya mwaka 2013 ambayo nimewawekea hapo juu, ndiyo utaratibu
waliofuata.
Pia walieleza kuwa sikuwa naifahamu na nilidanganywa kwani Kanuni
ilishabadilishwa. Mabadiliko haya ambayo ni katika kipengele (d) kuhusu hatua
ya dharura iliyochukuliwa na Kamati Kuu haikugusa kipengele (a) cha Kanuni.
Yaani ni kuwa hata kama Kamati kuu itachukua hatua ya dharura kwa mujibu wa
kipengele (d), bado kipengele (a) ni lazima ifuatwe na inatamka wazi sharti la
kiongozi kupewa mashtaka kwa maandishi na kupewa nafasi ya kujibu kwa
maandishi.
Hii ni haki ya msingi kwa kila utawala au uongozi.
Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe hakupewa mashtaka yake aliyakuta ndani ya
kikao baada ya kupewa taarifa kwa ujumbe wa simu (text message au sms).
Kwa uzito wa makosa hayo yaliyosababisha kuvuliwa uongozi na kwa
kuangalia athari zake kwake yeye binafsi na chama kwa ujumla, Kamati Kuu
ilitakiwa kujiridhisha kwamba Kanuni za Uendeshaji na Katiba zinafuatwa.
Hili linaendana na utaratibu uliotumika kwa Samson Mwigamba kuvuliwa
nyadhifa yake ya uenyekiti wa mkoa. Yeye hakuitwa kabisa kwenye kikao hicho na
ni ukiukwaji wa Kanuni ya Uendeshaji Taarifa kwa
Vyombo vya habari 11/12/2013 Albert Msando 4
6.5.6(d) niliyoisoma hapo juu kwamba lazima kiongozi huyo aitwe
kwenye kikao.
Sababu zilizotumika ingawaje hajapokea taarifa rasmi ya maandishi kwa
mujibu wa Kanuni za Uendeshaji ni kwamba yeye ameshirki kwenye kuandaa na
kusambaza waraka ambao unasemekana ni mkakati wa ushindi wenye lengo la
kupindua uongozi uliopo.
Waraka huo haukumtaja Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe kama muandaaji au
msambazaji. Waliouandaa hawajaukana na badala yake wamesema waziwazi kabisa kwa
maneno na maandishi kwamba Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe HAHUSIKI. Sio sawa
kumuadhibu Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe kwa hisia au tu kwa sababu ya urafiki
wake na watu fulani.
Haya ni mapungufu ambayo kwa bahati nzuri Katiba na Kanuni za Uendeshaji
zinatoa nafasi ya kurekebishwa kwa kutoa nafasi ya kukata rufaa. Na utaratibu
ni huu hapa;
Kwa ufupi, Ibara 6.3.6(d) ya Katiba ya Chama; “Kiongozi
aliyechukuliwa hatua za kinidhamu na mamlaka yake ya nidhamu anayo haki ya kukata rufaa ngazi ya juu ya ile mamlaka
yake ya nidhamu na uamuzi wa ngazi hiyo utakuwa wa mwisho”.
Taarifa kwa Vyombo vya habari 11/12/2013 Albert Msando 5
Ibara 6.3.6(e) ya Katiba ya Chama; “Rufaa yoyote lazima
ifanyike katika muda wa siku thelathini tangu tarehe ya kupokea rasmi kwa maandishi maamuzi ya mamlaka iliyotoa
adhabu”.
Kanuni za Uendeshaji zinatoa UTARATIBU ambao unatakiwa ufuatwe ili
kiongozi aliyeadhibiwa aweze kutumia HAKI yake ya kukata rufani kwa maneno
haya; Kanuni ya 6.5.8 ya Kanuni za Uendeshaji;
“Kiongozi aliyeadhibiwa atapewa taarifa ya msingi wa maamuzi ya mamlaka ya
nidhamu ili kumuwezesha kuamua kukata rufani au la”
Kanuni ya 6.5.9 ya Kanuni za Uendeshaji; “Mwadhibiwa atakayeamua
kukata rufani atatakiwa kufanya hivyo katika muda wa siku thelathini baada ya kuarifiwa uamuzi wa
adhabu”
Kanuni ya 6.5.10 ya Kanuni za Uendeshaji; “Baada ya kutoa uamuzi
kikao husika kinalazimika kuandaa taarifa kamili ya mwenendo wa shauri na kuwasilisha ngazi ya juu. Taarifa
hiyo lazima ifike katika muda wa siku kumi na nne baada ya kikao cha
mamuzi”
Taarifa kwa Vyombo vya habari 11/12/2013 Albert Msando 6 Mpaka hivi sasa
hatujpokea taarifa kamili ya mwenendo wa shauri tokea kikao cha Kamati Kuu cha
tarehe 20-21/11/2013 Huo ndio utaratibu ambao Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe
ameamua kufuata kwa kuheshimu maamuzi ya Kamati Kuu lakini kukatia rufaa maamuzi hayo. Kuheshimu maamuzi sio kuyakubali
uhalali wake.
Kumekuwa na matukio ya kusikitisha ambayo mengine yamefikia mahali kuwa
fujo na vurugu ikiwa ni pamoja na kurushiwa mawe Katibu Mkuu wa Chama. Vurugu
hizo baadhi zimehusishwa na Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe na baadhi ya
watu.
Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe hahusiki kwa njia yoyote na hayo
yanayoendelea na anayakemea na kuwashauri wanachama wote kuwa watulivu na
kuendelea kuwaheshimu viongozi wa kitaifa. Hatua zimeshachukuliwa kukata rufaa
na ni imani yake kwamba Baraza Kuu la Chama litatenda haki kwa
kupitia rufaa yake na kutoa uamuzi.
Nawashukuru wote.
ALBERT MSANDO, Mwanasheria
11/12/2013 .
No comments:
Post a Comment