![]() |
Former
president Nelson Mandela's body touched down at the Mthatha Airport at 1.37pm
on Saturday. He was given full military honours at Mthatha Airport. Picture:
eNCA.
|
![]() |
Former
president Nelson Mandela's body touched down at the Mthatha Airport at 1.37pm
on Saturday. Picture: eNCA
|
![]() |
Former
president Nelson Mandela's body touched down at the Mthatha Airport at 1.37pm
on Saturday. He was given full military honours at Mthatha Airport. Picture:
eNCA
|
![]() |
Former
president Nelson Mandela's body touched down at the Mthatha Airport at 1.37pm
on Saturday. He was given full military honours at Mthatha Airport. Picture:
eNCA
|
![]() |
The airforce
C-130 Hercules aircraft carrying former president Nelson Mandela's body touched
down at the Mthatha Airport at 1.37pm on Saturday. Picture: eNCA
|
![]() |
Former
president Nelson Mandela's body touched down at the Mthatha Airport at 1.37pm
on Saturday. He was given full military honours at Mthatha Airport. Picture:
eNCA.
|
Ng'ombe dume (fahali) atachinjwa kisha kuwekwa katika
kaburi atakamozikwa Rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini, Mzee Nelson
Mandela, Kijiji cha Qunu, Mthatha Jimbo la Eastern Cape Jumapili hii(Desemba
15,2013).
Viongozi wa
kimila wa Kabila la AbaThembu wametoa mwito kwa Serikali ya Afrika Kusini
isiingilie taratibu za mazishi ya kiongozi huyo na kuonya kwamba ikifanya
hivyo, 'Mandela hatapokewa na miungu' na kwamba roho yake inaweza kurejea na kuathiri
familia.
![]() |
The
motorcade escorting the body
the Nelson
Mandela ahead of his State
funeral,
passes through Mthatha
enroute to Qunu, where he will be buried. |
"Jumapili
baada ya mwili wake kuwekwa katika kaburi lake, taratibu zote za kimila
zitafanywa na Himaya ya Kifalme," alisema Kiongozi wa Jamii ya Xhosa, Nokuzola Mndende baada ya kutembelea
familia ya Mandela, nyumbani kwao Houghton, Johannesburg na kuongeza:
"Zitakuwa
ni mila na desturi za jadi, Serikali inapaswa kutupa nafasi na isituingilie.
Fahali (ng'ombe dume) atachinjwa kwa ajili ya kumsindikiza, ni familia ya
Mandela pekee watakaohusika na taratibu hizi za kumwandalia safari njema."
Mandela
anazaliwa katika Kabila la AbaThembu ambalo linazungumza Ki- Xhosa na kwa
mujibu wa taratibu za kabila hilo, hata mwili wake utashushwa kaburini na
viongozi wa kimila.
Hata hivyo,
habari zaidi kutoka Qunu zinasema licha ya taratibu za kimila, pia kutakuwapo
taratibu za Dini ya Kikristo, ambayo Mandela alikuwa muumini wake.
Jumamosi
Decemba 14, mwili wa Mandela ulisafrishwa kutoka Uwanja wa Ndege wa Jeshi wa
Waterkloof, Pretoria hadi Mthatha, Eastern Cape kwa ajili ya mazishi leo Jumapili.
Viongozi wa
juu wa Chama Tawala cha ANC, nao walitoa heshima za mwisho muda mfupi kabla ya
mwili huo kusafirishwa.
Taarifa ya
Idara ya Habari na Mawasiliano ya Afrika Kusini (GICS), ilisema Jeshi la Afrika
Kusini (SANDF), ndilo litakaloongoza shughuli zote za kuagwa kwa mwili wa
Mandela.
Mazishi
rasmi ya jumapili yatahudhuriwa na watu kama elfu tano hivi wakiwemo pia
viongozi mashuhuri wa kimataifa ikiwa ni pamoja na mwanamfalme Charles wa
Uingereza.
"Kamera
hazitaruhusiwa wakati wa mazishi, familia haitaki watu waone maiti itakapoteremshwa
kaburini," amesema msemaji wa serikali Phumla William.
Vyombo vya
habari na wageni wa hishma hawatoweza kuhudhuria, amesisitiza.
Hitimisho la
siku 10 za maombolezo ya msiba wa Mandela itakuwa Jumapili, Desemba 15 wakati
kiongozi huyo atakapozikwa katika makaburi ya familia.
Wakati wa
mazishi SANDF pia wamepewa jukumu la kusimamia upelekaji jeneza makaburini na
heshima za kitaifa zitatolea pamoja na wimbo wa Taifa kupigwa kabla ya maziko.
No comments:
Post a Comment