Kipigo cha 6 – 3 kwa Arsenal kimefanya uongozi wa Arsenal upunguzwe uwe Pointi 3 tu na Man City huku Chelsea pengo lao na Arsenal kuwa Pointi 2 tu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, December 14, 2013

Kipigo cha 6 – 3 kwa Arsenal kimefanya uongozi wa Arsenal upunguzwe uwe Pointi 3 tu na Man City huku Chelsea pengo lao na Arsenal kuwa Pointi 2 tu.


 Wachezaji wa Manchester City wakishangilia ushindi wao dhidi ya Arsenal leo(Desemba 14,2013) na imeonyesha ni hatari kweli, baada ya jioni hii kuifumua Arsenal mabao 6-3 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England uliofanyika Uwanja wa Etihad.


Theo Walcott alirejea uwanjani kwa mara ya kwanza leo tangu Septemba na akafunga mabao mawili ya Arsenal dakika za 31 na 63, wakati lingine lilifungwa na beki Per Mertesacker dakika ya 90.


Mabao ya Manchester City  yamefungwa na Sergio Aguero dakika ya 14, Alvaro Negredo dakika ya 39 Fernandinho mawili dakika za 50 na 88 David Silva dakika ya 66 na Yaya Toure dakika ya 90.


Vinara wa Ligi Kuu Uingereza, Arsenal leo (Desemba 14,2013) huko Jijini Manchester Uwanjani  Etihad wamebamizwa na Manchester City Bao 6-3 katika Mechi ambayo City waliitawala kabisa.

Kipigo hiki kimefanya uongozi wa Arsenal upunguzwe uwe Pointi  3 tu na Man City kukamata Nafasi ya tatu huku  Chelsea wakaweza kuwapiku baada ya kuifunga Crystal Palace bao 2-1 na kufanya pengo lao na Arsenal kuwa Pointi 2 tu.

Hiki ni kipigo cha 3 kwa Arsenal katika Ligi baada kufungwa 3-1 na Aston Villa ndani ya Emirates katika Siku ya Ufunguzi wa Msimu na kisha kuchapwa 1-0 na Mabingwa Man United Uwanjani Old Trafford.

Nyota wa Mechi hii ni Mbrazil Fernandinho ambae alinyakuwa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mechi na pia kupiga Bao 2.

Man City wameendeleza wimbi lao la kumimina mvua za Magoli Uwanjani kwao Etihad na sasa imepiga Bao 22 katika Mechi zao 4 zilizopita kwa kuichapa Swansea City 3-0, kuifumua Tottenham 6-0, kuirarua Norwich City 7-0 na leo kuwabomoa Arsenal Bao 6-3.

Latest Football

Mechi inayofuata kwa Arsenal kwenye Ligi ni Nyumbani kwao Emirates watakapopambana na Chelsea hapo Desemba 23.

As It Stands Table


Position Team Played Goal Difference Points
1 Arsenal 16 16 35
2 Chelsea 16 14 33
3 Man City 16 29 32
4 Everton 16 12 31
5 Liverpool 15 16 30
6 Newcastle 16 -1 27
7 Tottenham 15 -1 27
8 Southampton 16 5 24
9 Man Utd 15 3 22
10 Swansea 15 1 19
11 Aston Villa 15 -2 19
12 Hull 16 -6 19
13 Stoke 16 -5 18
14 Cardiff 16 -10 17
15 Norwich 15 -14 17
16 West Brom 16 -5 15
17 West Ham 16 -6 14
18 Crystal Palace 16 -13 13
19 Fulham 16 -15 13
20 Sunderland 16 -18 9


RATIBA

[Saa za Bongo]

Jumapili Desemba 15,2013.

16:30 Aston Villa v Man United
16:30 Norwich v Swansea
19:00 Tottenham v Liverpool

1 comment:

Post Bottom Ad