Miss Ngara 2013/2014 ni December 31,2013 Katika Ukumbi wa New Happy na Mkuu wa wilaya ya Ngara Bw.Costantine Kanyasu mgeni rasmi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, December 29, 2013

Miss Ngara 2013/2014 ni December 31,2013 Katika Ukumbi wa New Happy na Mkuu wa wilaya ya Ngara Bw.Costantine Kanyasu mgeni rasmi.

Shindano la kumsaka Miss  Ngara 2013/2014 lina elekea ukingoni ambapo Mshindi wa shindano hilo atapatikana siku ya mkesha wa Mwaka  washiriki kumi kutoka maeneo mbalimbali katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera  wamejitokeza na kwa sasa wako kambini mjini Ngara kwa ajili ya kufanya  maandalizi ya mwisho ya shindano hilo  ambalo pia litapambwa na burudani mbalimbali katika ukumbi wa New Happy(Desemba 31,2013).


Ili  kukamilisha shindano hilo  baadhi ya wadhamini  wamejitokeza kudhamini shindano la Miss Ngara 2013/2014 ambao mpaka sasa ni pamoja na PARADAISE HOTEL, HAPPY FASHION, Kampuni ya bia Tanzania (TBL) Kupitia bia yao ya CASTLE  LITE na COCA COLA.

Akiongea na Mwanawamakonda Blog Mmoja kati ya waandaaji  Happy Fashion(katikati katika picha) amewashukulu wadhamini hao ,Wazazi na Walezi wa Mabinti washiriki kwa kuwapa fursa ya kushiriki shindano la Miss Ngara pamoja na Mkuu wa wilaya ya Ngara Bw.Costantine Kanyasu kuwa nao bega kwa bega hasa  kwa kuwapa eneo la kupanda miti ikiwa ni harakati za utunzaji na uhifadhi wa mazingira  wilayani Ngara.

Picha juu na chini ni Washiriki 10 wa Miss Ngara 2013/2014 wakiwa katika picha mbalimbali za mapozi katika kambi yao mjini Ngara na Fainali za shindano hili ni December 31,2013 na mkuu wa wilaya ya Ngara  Bw.Costantine Kanyasu  anatajwa kuwa mgeni rasmi.



Fainali za shindano hili ni December 31,2013 na mkuu wa wilaya ya Ngara  Bw.Costantine Kanyasu  anatajwa kuwa mgeni rasmi.

Ili  kukamilisha shindano hilo  baadhi ya wadhamini  wamejitokeza kudhamini shindano la Miss Ngara 2013/2014 ambao mpaka sasa ni pamoja na PARADAISE HOTEL, HAPPY FASHION, Kampuni ya bia Tanzania (TBL) Kupitia bia yao ya CASTLE  LITE na COCA COLA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad