Dk.
Asha-Rose Mtengeti Migiro.
|
WANAWAKE
wengi nchini wameshika vyeo mbalimbali vya juu serikali au kwenye taasisi
binafsi.
Wafuatao
ni wanawake 10 ambao wanakalia au wamekalia vyeo hivyo hapa nchini kama
walivyomulikwa na Elvan Stambuli.
JULIET KARIUKI.
HUYU
ni Mkuruggenzi Mtendaji wa kwanza mwanamke katika Kituo cha Uwekezaji Tanzania
(TIC) . Uteuzi wake ulifanywa na Rais Jakaya Kikwete Aprili 12 mwaka huu na
akakabidhiwa ofisi siku hiyohiyo.
Bibi
Kariuki ana shahada ya kwanza ya sheria na ya uzamili, kwenye sheria ni mtalamu
wa ubia kati ya serikali na watu binafsi (Public Private Partnership). Aliwahi
kufanya kazi katika Chama Cha Mabenki ya Afrika Kusini.
MIZINGA
MELU.
NI Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC
tangu Machi 20 mwaka huu. Alichukua
nafasi hiyo kutoka kwa Lawrance Mafuru.
Ni mzaliwa wa Zambia katika Kijiji cha
Mazabuka na ana shahada ya juu ya biashara (MBA), Zambia National Commercial
Bank na Standard Chartered Bank.
SAUDA
S. RAJABU.
NAYE
ni mwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa juu wa Mkurugenzi Mkuu na Mtendaji Mkuu
(CEO) wa Kampuni ya Ndege ya Precision Air hapa nchini.
Alianza kutumikia
nafasi hiyo Machi Mosi, mwaka huu baada ya aliyekuwa akikalia kiti hicho,
Alfonce Kioko kumaliza muda wake.
Ana
shahada ya kwanza ya biashara na sasa yupo mbioni ‘kuchimbua’ shahada ya juu ya
biashara. Amewahi kufanya kazi katika mashirika mengine ya ndege kama vile
Kenya Airways na ya Rwanda na Burundi.
Add caption |
ANNE
MAKINDA.
NI
mwanamke wa kwanza nchini kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, alichukua nafasi hiyo kutoka kwa Samwel Sitta ambaye aliliendesha
Bunge kwa msimu mmoja tu mwaka 2005 hadi 2010.
Makinda
amevunja rekodi kwa kukaa bungeni kwa miaka mingi kwani alianza kuwa Mbunge wa
Jimbo la Njombe mwaka 1975 hadi leo. Tayari ametangaza kung’atuka (2015).
BALOZI
LIBERATA MULAMULA.
NI
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico. Amewahi kuwa balozi wetu nchini
Canada kuanzia mwaka 1999 hadi 2002.
Amewahi kuteuliwa kuwa mmoja wa
wasuluhishi wa mgogoro wa Rwanda. Ni msomi mwenye shahada ya kwanza na ya pili
ya sanaa,alisomea Chuo Kikuu cha St. John’s, Marekani, 1989.
MCHUNGAJI
G.RWAKATARE.
HUYU
ni Mchungaji na kiongozi wa Kanisa la Mikocheni B Assemblies of God na
mwanzilishi wa shule za St. Mary’s
International alizozifungua mwaka 1997.
Licha
ya kazi ya kuhubiri Injili, Mama Rwakatare ana chombo cha habari ambacho ni
Praise
Power Radio 99.2 FM inayoelimisha jamii na kutoa burudani za kiroho.
GETRUDE
MONGELLA.
ALIKUWA
mwanamke wa kwanza kuwa Rais wa Bunge la Afrika, amewahi kuwa Balozi wa
Tanzania nchini India 1991 hadi 1992 na akawa Katibu Mkuu katika Mkutano wa
Wanawake Duniani uliofanyika Beijing, China
mwaka 1995.
Aliwahi
kuwa mshauri wa Mkurugenzi Mkuu wa Unesco na aliwatumikia wananchi wa Ukerewe
akiwa ni mbunge kuanzia 2000 hadi 2010 na Februari mwaka 2008 alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya African Press
Organization (APO).
ASHA
ROSE MIGIRO.
Asha-Rose
Mtengeti Migiro ni mwanasheria na mwanasiasa. Licha ya kufundisha sheria Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam, mama huyu aliwahi kuwa mwanamke wa kwanza kuwa Waziri wa
Mambo ya Nchi za Nje wa Tanzania.
Lakini kikubwa zaidi ni pale alipoteuliwa
kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Juni 2012.
Baada ya kumaliza muda
wake Umoja wa Mataifa, Migiro hivi sasa yupo nchini akiongoza kitengo cha Mambo
ya Nchi za Nje cha Chama Cha Mapinduzi.
SUSAN
MASHIBE.
HUYU
ni rubani na ni injinia wa ndege, hivyo kuwa mwanamke wa kwanza nchini kuwa na
elimu hizo alizopatia Chuo Kikuu cha Michigan, Marekani.
Ni Mwanzilishi na
kiongozi wa Tanzanite Jet Centre Ltd, kampuni aliyoianzisha mwaka 2003 ambayo
sasa inajulikana kama Via Aviation na inajishughulisha na biashara ya mambo ya
anga nchini na barani Afrika.
Alikutana na Rais Barrack Obama alipokuja nchini
hivi karibuni.
JOYCE
MHAVILE.
NI
Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Radio One kuanzia 1994. Amekiongoza kituo hicho
cha runinga hadi kushika nafasi ya kwanza kwa ufanisi mwaka jana.
Amebobea
kwenye taaluma ya uandishi wa habari.
Ni
mmoja wa wanawake katika Bara la Afrika walioongoza chombo cha habari kwa
mafanikio na kuwa mfano kwa wasichana wanaochipukia hivi sasa katika nchi yetu.
No comments:
Post a Comment