Tazama Picha zaidi za Gari lililotengenezwa na Mtanzania na robu tatu ya vitu vilivyotengeneza ni Mbao na inatumia mafuta lita moja kwa kilomita nane. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, July 14, 2013

Tazama Picha zaidi za Gari lililotengenezwa na Mtanzania na robu tatu ya vitu vilivyotengeneza ni Mbao na inatumia mafuta lita moja kwa kilomita nane.


Keneth  Mwang'oka akiwa ndani ya gari lake ,Gari ya mbao iliyobuniwa na mkazi huyo wa kijiji cha Nyololo mkaoni Iringa, na imeelezwa kwamba gari hilo limeokoa shilingi Bilioni moja kwa mwaka kwa kuhamasisha kuhifadhi mazingira katika msitu wa Sao Hill ulioko mkoani humo.



Umeuona mlango? Mwang'oka akishuka garini wakati wa Maonesho ya 37 ya Sabasaba yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam mwaka huu 2013).


Akifunga mlango wa Gari hilo aina ya Toyota Hiace aliinunua kutoka kwa mtu ambaye alitaka kuiuza kama chuma chakavu na aliitengeneza ili iweze kusaidia katika kuwavutia wanajiji na kupata njia ya kuwapata kwa urahisia wanakijiji  kufikisha ujumbe wa kuhifadhi Misitu na Mazingira.


Mwangoka ambaye ni fundi wa gari hiyo, Hapa Akionyesha siti ya abiria wake na anasema  gari hiyo ina injini ya Toyota 1S, robu tatu ya vitu vilivyotengeneza ni mbao na inatumia mafuta lita moja kwa kilomita nane.


Mwangoka anasema kwa juu kuna roof ya kupitisha upepo.



Kwa ndani ……Umeona dashboard yake ilivyo ambapo robu tatu ya vitu vilivyotengeneza ni mbao.


Mbunifu Kenneth Joseph Mwang'oka akiwa katika pozi  ndani ya gari lake hilo likiwa  katika viwanja vya Maonesho ya 37 ya Sabasaba yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam  mwaka huu 2013.


Gari hilo linaloonekana kwa mbele ambapo robu tatu ya vitu vilivyotengeneza ni mbao.




Watu wakilishangaa gaari hilo Mbunifu gari hilo likiwa  katika viwanja vya Maonesho ya 37 ya Sabasaba hivi karibuni  jijini Dar es Salaam  mwaka huu 2013.


Umeona vitendea kazi vyake vilivyo na inatumia mafuta lita moja kwa kilomita nane.


Usukani wake ni mbao tu kweli Misitu yetu ni mali.


Muonekano wa gari hilo kwa nyuma likiwa katika viwanja vya Maonesho ya 37 ya Sabasaba hivi karibuni  jijini Dar es Salaam  mwaka huu 2013.


Keneth  Mwang'oka akiwa ndani ya gari lake ,Gari ya mbao iliyobuniwa na mkazi huyo wa kijiji cha Nyololo mkaoni Iringa  anasema hata rivasi kama kawa unaliendesha tu.


Ama kweli TANZANIA  imejaliwa watu wenye vipaji na ujuzi mkubwa katika nyanja ya Sayansi na Teknolojia ila kuna vitu vidogo vinavyowakwaza kusimama na kwenda sambamba na wataalam wa mataifa mengine ambao wapo mbali katika suala la vipaji na ubunifu.



Mifano michache ni watu wanaomudu kutengeneza magobole, mashine mbalimbali na vitu vingine na hata wabunifu wa mrusho wa matangazo ya radio, ambao badala ya kuwezeshwa hupata vikwazo ikiwamo kunaswa na vyombo vya dola na kufunguliwa mashtaka ilihali wangeweza kutumika kuitangaza Tanzania.



Hapo juu ni mmoja wa wabunifu wa Kitanzania aliyeweza kutengeneza gari ambalo alitumia muda wa miezi sita kulikamilisha kwa kuokoteza vifaa na kulipamba kiasilia kwa kutumia malighafi ya misitu.



Majina yake kamili ni Kenneth Joseph Mwang'oka ambaye alikuwa moja ya vivutio katika Maonyesho ya Biashara ya Sabasaba kwa ubunifu wa gari hilo linalotumia injini ya Toyota na kuongeza ubunifu wao kiasi kwamba gari hilo lililomgharimu kiasi cha Sh Milioni 8.6 kutembea kutoka sehemu mbalimbali nchini.



Mwenyeji huyo wa mkoa wa Mbeya, lakini ubunifu wake kaufanyia mjini Iringa anasema lengo lake ni kuhakikisha anakuja kutengeneza vitu zaidi ya gari hilo la aina yake.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad