Chadema yaitesa CCM uchaguzi wa Udiwani kwenye kata nne za Jimbo la Arusha Mjini . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, July 15, 2013

Chadema yaitesa CCM uchaguzi wa Udiwani kwenye kata nne za Jimbo la Arusha Mjini .



CHADEMA.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), `kimefunika' katika uchaguzi mdogo wa madiwani uliofanyika kwenye kata nne za Jimbo la Arusha Mjini uliofanyika jana(Julai 14,2013).




Matokeo katika vituo mbalimbali vya kata hizo nne ambayo kwa mujibu wa   Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), yalionyesha Chadema ikiongoza kwa idadi kubwa ya kura zilizopigwa kwenye vituo 136 vya kupigia kura huku kikifuatiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).



Matokeo kamili katika vituo hivyo yalikuwa kama ifuatavyo:-





Katika Kata ya Elerai, mgombea wa CHADEMA Injinia Jeremia Mpinga alimbwaga Emanueli Laizer wa CCM kwa kura 1,715, dhidi ya 1,239.




Kata hiyo ilikuwa na wapiga kura 23,797 waliojiandikisha na vituo 55 vya kupigia kura, lakini idadi kubwa ya wananchi hawakujitokeza.




Matokeo ya kura yalitangazwa chini ya ulinzi mkali wa askari polisi zaidi ya 40 wenye silaha, na kupokelewa kwa shangwe kubwa na wafuasi na mashabiki wa CHADEMA.




Katika Kata ya Kaloleni, mgombea wa CHADEMA, Kessy Emmanuel Miliare alimshinda kwa mbali mgombea wa CCM kwa kura 1,470 dhidi ya 530, wakati mgombea wa CUF ameambulia kura 275. waliojiandikisha 12,674 waliopiga kura 2,292. Kura halali ni 2,277 na zilizoharibika 15.




Akitangaza matokeo katika Kata ya Themi, Msimamizi wa Uchaguzi, Editha Mboye alimtangaza mgombea udiwani wa CHADEMA, Mallance Kinabo kuwa mshindi kwa kupata kura 678, akimwacha mbali mgombea wa CCM Victor Mkolwe aliyepata kura 326, huku yule wa CUF, Lebora Ndervai akipata kura 313.




Wafuasi wa CHADEMA.
Kata ya Kimandolu, CHADEMA pia wameibuka na ushindi mkubwa na kuiacha vibaya CCM.




Mgombea wa CHADEMA, Elishadai Ngowi amemshinda mgombea wa CCM, Edina Sauli kwa kura 2,265, dhidi ya 1,169 za mpinzani wake.




Mara baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Jiji la Arusha lilizizima kwa shangwe na nderemo, huku idadi kubwa ya watu wakijipongeza kwa ushindi huo mkubwa.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad