Mkoa wa Kagera,unakabiliwa na wimbi la wahamiaji haramu wanaokadiriwa kufikia 32,000. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, July 14, 2013

Mkoa wa Kagera,unakabiliwa na wimbi la wahamiaji haramu wanaokadiriwa kufikia 32,000.



Baadhi ya wahamiaji Haramu wanaosadikiwa kutoka nchini Jirani ya Burundi  wakiwa kwenye gari la Idara ya Uhamiaji wilaya ya Ngara tayari kurudishwa kwao nchini Burundi baada ya kukamatwa katika Mpaka wa Kabanga wilayani Ngara mkoani Kagera hivi karibuni.
Gari  la Idara ya Uhamiaji wilaya ya Ngara likiwa limewababe Baadhi ya wahamiaji Haramu wanaosadikiwa kutoka nchini Jirani ya Burundi  tayari kurudishwa kwao nchini Burundi baada ya kukamatwa katika Mpaka wa Kabanga wilayani Ngara mkoani Kagera hivi karibuni.
Mkoa wa Kagera,unakabiliwa na wimbi la wahamiaji haramu wanaokadiriwa kufikia 32,000 ambao huingia njia za panya.



Naibu Kamishina wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kagera George Kombe aliiambia MTANZANIA mjini Bukoba jana(Julai 13,2013).



Alisema wahamiaji hao, wanaingia mkoani Kagera kupitia maeneo ya Murongo, Kanyigo, Rusumo, Mtukura, Bugango na Kabanga mkoani Humo.



Alisema kutokana na kuwepo kwa wahamiaji hao, idara yake inakadiria kutumia Shilingi Milioni 650, kwa ajili ya kufanya operesheni ya kuwarudisha makwao.



Alisema wahamiaji wengi, wanatoka nchi za Rwanda, Burundi, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC).



Alisema pamoja na idadi hiyo, bado wanaendelea na kazi ya kuwatambua wahamiaji wengine.



Alisema, pamoja na jitihada hizo, bado kuna baadhi ya viongozi wakiwamo wenyeviti wa vitongoji ambao wanawahifadhi majumbani mwao.



Alisema mwaka 2006, walifanya operesheni kama hiyo ambapo walitumia Sh milionin 450.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad